2022
Mihutasari ya Mkutano
Novemba 2022


“ Mihutasari ya Mkutano,” Rafiki, Novemba 2022, 5.

Mihutasari ya Mkutano

Kila Mmoja Anaweza Kutumikia

Picha
Dallin H. Oaks

Rais Oaks alishiriki hadithi ya mtu anayeitwa Bwana Gabriel, aliyewasaidia maelfu ya watoto wakimbizi. Alitengeneza “shule za miti,” ambapo watoto walikusanyika kwa ajili ya masomo chini ya kivuli cha miti. Alipoona hitaji, alisaidia! Mungu huwahamasisha watu wengi kama Bwana Gabriel kutenda mema.

Hili hunifunza:

Kushiriki Kitabu cha Mormoni

Picha
Ronald A. Rasband

Mzee Rasband alisimulia jinsi nabii alivyompa mfalme huko Ghana nakala ya Kitabu cha Mormoni. Kwa pamoja, Rais Nelson na mfalme walisoma kuhusu Yesu Kristo katika 3 Nefi 11. Mfalme alisema kitabu kilikuwa cha thamani kuliko almasi au rubi kwa sababu kilimfunza zaidi kuhusu Yesu.

Hili hunifunza:

Jibu ni Yesu

Picha
Mzee Ryan K. Olsen

Mzee Olsen alizungumza kuhusu mpwa wake Nash. Walikuwa wakifanya kazi pamoja wakati Nash alipokuja na wazo maridadi la kutatua tatizo. Mzee Olsen alimuuliza Nash aliwezaje kujua hilo. Nash alijibu, “Yesu.” Yesu Kristo ndiye jibu kwa matatizo yetu yote.

Hili hunifunza:

Miwani ya Kuona

Picha
Dada Tracy Y. Browning

Dada Browning alisema kwamba alihitaji miwani kumsaidia kuona. Kila asubuhi, kitu cha kwanza anachofanya ni kuichukua miwani yake. Alieleza kuhusu jinsi anavyomuhitaji Yesu Kristo kila siku kama vile anavyohitaji miwani yake. Mwokozi ameahidi kutuongoza na kutuelekeza wakati tunapotenga muda kwa ajili Yake.

Hili hunifunza:

Chapisha