2022
Onyesha na Elezea kutoka kwenye Mkutano
Novemba 2022


“Onyesha na Elezea kutoka kwenye Mkutano,” Rafiki, Novemba 2022, 6–7.

Onyesha na Elezea kutoka kwenye Mkutano

Picha
Sophie, Bailey na Clair B. wakiwa na hekalu la mchemraba wa sukari

Sophie, Bailey na Claire B., miaka 4, 8 na 6, kutoka Texas, Marekani, walitengeneza mahekalu kwa kutumia mchemraba wa sukari wakati wakisikiliza mkutano.

Picha
Fabiola R. akiwa karibu na TV ikimuonyesha Rais Henry B. Eyring akizungumza

Fabiola R., miaka 12, kutoka Rio Grande do Sul, Brazil, hupenda kusikiliza mkutano pamoja na familia yake. Hawezi kusoma wala kuzungumza lakini huisi amani na upendo kutoka kwenye jumbe za mkutano. Sehemu anayoipenda sana ni kumsikiliza rafiki yake, Rais Henry B. Eyring.

Picha
Mchoro wa mtoto kuhusu Yesu Kristo

Liesel L., miaka 9, Kansas, Marekani

Picha
Lucy M. akiwa na mandhari ya mkutano mkuu iliyotengenezwa kutokana na maboksi ya plastiki

Lucy M., miaka 7, Utah, Marekani

Picha
Mchoro wa mtoto wa wazungumzaji wa mkutano mkuu

Milo M., miaka 8, Arizona, Marekani

Picha
Manu L.

Tunacheza mchezo wakati wa mkutano mkuu. Tunaweka kibandiko kwenye kipande cha karatasi kila mara tunaposikia jina la Kristo. Karatasi zetu huishia kujaa vibandiko!

Manu L., miaka 6, Tel Aviv, Israel

Picha
Adam L.

Napenda hadithi za kupendeza ambazo nabii na mitume hutuhadithia kuhusu maisha yao.

Adam L., miaka 9, Tel Aviv, Israel

Picha
Reuben F.

Napenda muziki! Sehemu yangu pendwa ni kusikiliza kwaya ikiimba. Natumaini nitaimba kwenye kwaya siku moja.

Reuben F., miaka 4, Louisiana, Marekani

Picha
Isaac E.

Napenda kumsikiliza nabii wetu na nyimbo maalumu za dini zinazoimbwa na Kwaya ya Tabenako.

Isaac E., miaka 6, Jimbo la Magharibi, Ghana

Picha
William S.

Napenda kuwa na familia yangu na kupaka rangi picha wakati wa mkutano mkuu.

William S., miaka 7, Tasmania, Australia

Picha
Noah A.

Napenda kumsikiliza nabii wetu na kusikia wapi mahekalu mapya yatajengwa.

Noah A., miaka 12, Al-Ahmadi, Kuwait

Picha
Danielle, Hailey na Robin L.

Tunapenda kusikiliza kwaya ikiimba na kufanya shughuli za mkutano.

Danielle, Hailey na Robin L., miaka 6, 10 na 9, Singapore

Chapisha