2010–2019
Ripoti ya Idara ya Ukaguzi ya Kanisa, 2018
Mkutano Mkuu wa Aprili 2019


2:3

Ripoti ya Idara ya Ukaguzi ya Kanisa, 2018

Kwa Urais wa Kwanza wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho

Ndugu Wapendwa: Kama tulivyoelekezwa na ufunuo uliorekodiwa katika sehemu ya 120 ya Mafundisho na Maagano, Baraza la Mpangilio wa Zaka—linalojumuisha Urais wa Kwanza, Akidi ya Mitume Kumi na Wawili, na Uaskofu Simamizi—huidhinisha matumizi ya fedha za Kanisa. Mashirika ya Kanisa hugawa fedha kwa mujibu wa bajeti, sera, na taratibu zilizoidhinishwa.

Idara ya Ukaguzi ya Kanisa, inayojumuisha wataalamu walioidhinishwa na inayojitegemea kutoka kwenye idara zingine zote za Kanisa, ina wajibu wa kufanya ukaguzi kwa lengo la kutoa uhakika kuhusu michango iliyopokelewa, matumizi yaliyofanywa, na ulinzi wa mali za Kanisa.

Kwa mujibu wa ukaguzi uliofanywa, Idara ya Ukaguzi ya Kanisa inatoa maoni kwamba, katika mambo yote muhimu, michango iliyopokelewa, matumizi yaliyofanywa, na mali ya Kanisa kwa mwaka 2018 vimerekodiwa na kusimamiwa kwa mujibu wa bajeti ya Kanisa, sera, na utendaji wa uhasibu ulioidhinishwa. Kanisa linafuata utendaji uliofundishwa kwa waumini wake wa kuishi ndani ya bajeti, kuepuka madeni, na kuweka akiba kwa ajili ya wakati wa shida.

Kwa heshima imewasilishwa,

Idara ya Ukaguzi ya Kanisa

Kevin R. Jergensen

Mkurugenzi Mtendaji