NJIA YANGU YA AGANO
Jifunze kuhusu Ukuhani wa Melkizedeki
“Niko hivi nilivyo leo kwa sababu ya injili hii ya kupendeza iliyorejeshwa ambayo ninayo katika maisha yangu.”
“Na ukuhani huu mkuu huihudumia injili na hushikilia ufunguo wa siri za ufalme, hata ufunguo wa ufahamu wa Mungu” (Mafundisho na Maagano 84:19).
“Niko hivi nilivyo leo kwa sababu ya injili hii ya kupendeza, iliyorejeshwa ambayo ninayo katika maisha yangu.” Dada Khosi Ndlovu wa kata ya Tsakane anapata shangwe wakati anapofikiria kuhusu jinsi ukuhani ulivyobariki maisha yake. Anaendelea, “Kupitia nguvu ya Ukuhani wa Melkzedeki injili hii ya urejesho, mafundisho, maonyo na ufunuo unaopokelewa na Nabii vimenijenga na kuendelea kunijenga kuwa mtu ambaye Baba anataka mimi niwe.”
Kupitia Ukuhani wa Melkizedeki, kila muumini wa Kanisa anaweza kupokea ibada za ukuhani. Ibada hizi hutusaidia kufanya maagano pamoja na Mungu.
Wenye Ukuhani wa Melkizedeki wanaweza kutoa baraka ya faraja na kuwabariki wagonjwa. Baraka hizi zinaweza kuleta ahueni kubwa na faraja pale inapohitajika.
Wakati wanawake na wanaume wote hutenda chini ya nguvu ya UKuhani wa Melkizedeki pale wanapohudumu ndani ya Kanisa, wanaume watu wazima wenye kustahili wanatawazwa kwenye Ukuhani wa Melkizedeki na kutekeleza ibada za ukuhani.
Rais Dallin H. Oaks amesema, “Ukuhani ni nguvu takatifu na mamlaka yanayoshikiliwa katika uaminifu ili yatumike kwa ajili ya kazi ya Mungu kwa manufaa ya watoto Wake wote. . . .
“Baraka za ukuhani, kama vile utimilifu wa injili na ibada kama ubatizo, uthibitisho na kupokea kipawa cha Roho Mtakatifu, endaumenti ya hekaluni na ndoa ya milele vinapatikana kwa wanaume na wanawake pia.”1
Dada Khosi anasema kwamba “katika siku na zama hizi, katika ulimwengu huu uliojaa machafuko tunao akina kaka ambao jukumu lao kuu ni kutuinua, kutuendeleza na kutusaidia kuwa kile Baba yetu anataka sisi tuwe. Ni shangwe na faraja iliyoje kwangu. Nina furaha kujua kwamba kupitia Ukuhani wa Melkizedeki milango ya ufalme wa selestia imefunguliwa kwa wote.”