2022
July 1847: Waasisi Wanawasili katika Bonde la Salt Lake
Julai/Agosti 2022


MWEZI HUU KATIKA HISTORIA YA KANISA

July 1847: Waasisi Wanawasili katika Bonde la Salt Lake

Brigham Young (1801-1877), Rais wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili wakati wa mauaji ya nabii Joseph Smith, aliwaweka Watakatifu wa Siku za Mwisho katika makundi ambayo yangesafiri kuvuka Marekani na nyikani walipokuwa wakitafuta ardhi ambayo Watakatifu wangeishi kwa usalama na Kanisa lingeweza kuwakaribisha waumini kutoka ulimwenguni kote. Brigham alipajua mahali alipokuwa akipatafuta. Alipaona kwenye ono na alipoulizwa wapi alikuwa akienda, angejibu, “Nitawaonyesha wakati tutakapopafikia. Nimepaona, nimepaona kwenye ono na macho yangu ya nyama yatakapopaona mahali hapo, nitapajua.”1

Mnamo Julai 24, 1847, Brigham Young aliliona Bonde la Salt Lake kwa mara ya kwanza. EHe

Baada ya safari ya zaidi ya maili elfu moja kupita prairie, jangwa na makorongo makubwa, mwonekano ulikuwa wa kustaajabisha. Hapa palikuwa ni mahali ambapo Watakatifu wangeishi na kuanzisha kigingi kingine cha Sayuni. Wangeweza kujenga makazi, kulima mashamba ya matunda na mazao na kuwakusanya watu wa Mungu kutoka ulimwenguni kote. Na kabla ya muda kupita, nyumba ya Bwana ingeanzishwa katika milima na kuinuliwa juu ya vilima, kama Isaya alivyotabiri.2 Akiangaza angaza kwenye bonde, Brigham alilichunguza kwa dakika kadhaa na kusema “inatosha. Hapa ni mahali sahihi, endeleeni.”3

Ulimwenguni kote watu wameacha desturi zao za kidini na baadhi wameacha familia zao na nyumba zao ili kujiunga na Watakatifu wa Siku za Mwisho kama waasisi wa siku za leo, kama vile ilivyokuwa kwa Watakatifu wa mwanzo.

Mzee Dieter F. Uchtdorf alisema:

“Sina mababu miongoni mwa waasisi wa karne ya kumi na tisa. Hata hivyo, tangu siku za mwanzo za uumini wangu wa Kanisa, nimehisi undugu wa karibu na wale waasisi wa mwanzo waliovuka nyanda. Wao ni mababu zangu wa kiroho, kama walivyo kwa kila muumini wa Kanisa, bila kujali utaifa, lugha au utamaduni.”4

Kama waumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho, imani yetu huimarishwa kwa simulizi zilizorekodiwa na waasisi wa mwanzo na wa sasa. Hadithi zao za imani na ujasiri hutukumbusha baraka za injili ya Yesu Kristo na kutuhimiza kubakia kwenye njia ya agano.

Muhtasari

  1. David W. Evans, “Discourse by Elder Erastus Snow,” The Deseret News, 22 Oct. 1873, 4.

  2. Watakatifu, Juzuu ya 2, Sura ya 4, Kama Bendera kwa Mataifa, 32.

  3. Watakatifu, Juzuu ya 2, Sura ya 4, Kama Bendera kwa Mataifa, 34.

  4. Dieter F. Uchtdorf, “Heeding the Voice of the Prophets,” Ensign, July 2008, 5.