2022
Kuhudumu
Julai/Agosti 2022


DONDOO ZA KITABU CHA MAELEKEZO

Kuhudumu

Ni fursa iliyoje ya mimi na wewe kuwa akina kaka na akina dada wahudumu! Kitabu cha Maelekezo ya Jumla, Sehemu ya 21, kinatupatia ushauri wenye msukumo ili kutusaidia kufuata mfano wa Kristo katika kuhudumu.

Kuhudumu humaanisha kuwatumikia wengine kama Mwokozi alivyofanya. Aliwapenda, kuwafundisha, kuwaombea, kuwafariji na kuwabariki wale waliomzunguka.

Bwana anataka waumini wote wa Kanisa Lake kupokea matunzo kama hayo.

Kuhudumu hutusaidia kushika amri ya kumpenda Mungu na kuwapenda jirani zetu. Pia ni njia muhimu ya kusaidia kufanikisha kazi ya wokovu na kuinuliwa.

Urais wa akidi ya wazee na Muungano wa Usaidizi hutusaidia kujifunza jinsi ya kuwahudumia wengine na kutupatia uvuvio, mwongozo na msaada. wao pamoja na sisi tunaweza kutafuta mwongozo kutoka kwenye maandiko, sehemu hii ya (21) katika kitabu cha Maelekezo na kwenye tovuti www.ministering.ChurchofJesusChrist.org.

Tunamwakilisha Bwana. Tunawasaidia waumini kuhisi upendo na msaada wa askofu na Muungano wa Usaidizi au viongozi wa akidi. Tunawajali waumini na tu wamoja pamoja nao. Tunasaidia kuimarisha imani yao kwa Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo. Tunawasaidia watunze maagano matakatifu, kutambua mahitaji yao, kuwapa msaada na faraja na kuwasaidia kuwa wenye kujitegemea kiroho na kimwili. Tunaboresha jitihada zetu kwenye mahitaji ya kaka na dada zetu.

Mwokozi aliwapa wanafunzi Wake majukumu yenye tija. Katika njia sawa na hiyo, nasi tumepokea majukumu yenye tija ya kuhudumu kama Mwokozi alivyofanya. Basi na tufuate mfano wa Kristo na katika kufanya hivyo, sisi pamoja na kaka na dada zetu tutahisi upendo wa Mwokozi.

Chapisha