2022
Jitayarishe kwa ajili ya Hekalu!
Novemba 2022


Jitayarishe kwa ajili ya Hekalu!

Tuliwauliza watoto jinsi wanavyojitayarisha kwenda hekaluni na kile wanachotarajia. Hiki ndicho walichokisema!

Picha
Portrait of Alivia Woodbury.

“Ninajifunza maswali ya mahojiano ya kuingia hekaluni ili kuwa tayari kwenda hekaluni. Ninataka ushuhuda imara.”

Alivia W., umri miaka 9, Utah, Marekani

Picha
Picture of Luke Freeman.

“ Nina shauku ya kwenda hekaluni siku moja kufanya ubatizo. Nilijifunza mengi sana kuhusu hekalu kwa kujifunza maandiko. Nimehamasika kwa sababu hata ninapokuwa kwenye viwanja vya hekalu, ninaweza kuhisi Roho kwa nguvu sana. Nina uhakika nitamhisi Roho kwa nguvu zaidi nikiingia ndani.

Luke F., umri miaka 10, Idaho, Marekani

Picha
Picture of Mark Yeromin sitting on the couch holding a kitten.

“Unaweza kujiandaa kwa ajili ya hekalu kidogo kidogo kila siku. Ninazishika amri. Ninasoma maandiko pamoja na kaka na mama yangu kila asubuhi kabla ya shule. Ninajaribu kuwa mfano kwa ajili ya marafiki. Ninajaribu kuchagua mema kama inavyosemwa katika wimbo ‘Do What Is Right’ (Nyimbo za Kanisa, na. 237). Tunaimba huo asubuhi ili kuanza siku vyema!”

Mark Y., umri miaka 10, Poltava, Ukraine

Picha
Picture of Daniel Denshchykov.

“Ninasali kila siku na ninawauliza wazazi wangu kuhusu ibada za hekaluni. Pia ninajitayarisha kwa ajili ya mahojiano na askofu wangu. Ninashauku ya kwenda hekaluni.”

Daniel D., miaka 11, Kyiv, Ukrane

Picha
Picture of Antonella Igor.

“Nilipenda mara yangu ya kwanza kwenda hekaluni. Kabla ya zamu yangu kwa ajili ya ubatizo, nilihudumu kama shahidi. Nilipewa jukumu la kumwangalia mtu mwingine akibatizwa na nilihakikisha alizama kabisa ndani ya maji. Ilipofika zamu yangu kubatizwa, maji yalikuwa ya uvuguvugu. Nilihisi amani na furaha. Nalipenda hekalu na ninapenda kusaidia katika kazi hii kuu.

Antonella A., miaka 12, British Columbia, Canada

Chapisha