2023
Jinsi Unavyoweza Kuwa Mmisionari
Julai 2023


“Jinsi Unavyoweza Kuwa Mmisionari,” Rafiki, Julai 2023, 2–3.

Kutoka Urais wa Kwanza

Jinsi Unavyoweza Kuwa Mmisionari

Imetoholewa kutoka “Kuhubiri Injili ya Amani,” Liahona, Mei 2022, 6–7 na “Be Thou an Example of the Believers,” Liahona, Nov. 2010, 47–49.

Picha
Yesu Kristo akizungumza na wanafunzi Wake

Bwana aliwaambia wanafunzi Wake “enendeni … ulimwenguni mwote, mkaihubiri Injili kwa kila kiumbe.” (Marko 16:15). Kila mtu anastahili nafasi ya kujua wapi wanaweza kupata tumaini na amani ya Yesu Kristo. Kila mmoja wetu ana jukumu takatifu la kushiriki amani ya Yesu Kristo kwa wale wote ambao watasikiliza.

Unaweza kuwasaidia wengine wapate amani ya injili kwa:

  • Kuwa mfano mzuri.

  • Kumfuata Yesu Kristo ili kwamba nuru Yake iweze kung’ara katika macho yako.

  • Kutanua mduara wako wa marafiki.

  • Kumwalika rafiki asome Kitabu cha Mormoni.

  • Kumwalika rafiki aende kwenye mkutano au shughuli ya Kanisa pamoja nawe.

Unaweza pia kufanya uamuzi wa kuhudumu misheni wakati utakapokuwa mkubwa. Uamuzi huu utakubariki wewe pamoja na wengine wengi.

Mduara wa Marafiki

Picha
PDF ya hadithi

Vielelezo na Garth Bruner

Katika picha hapa chini, angalia ni marafiki wangapi kwenye shughuli ya Msingi wana:

  • Nywele nyeusi

  • Shati la njano

  • Nywele zilizosukwa

  • Miwani

  • Begi la mgongoni la kijani

  • Viatu vyekundu

  • Kiti mwendo

  • Mpira wa miguu

Chapisha