2023
Changamoto ya Umisionari
Julai 2023


“Changamoto ya Umisionari,” Rafiki, Julai 2023, 38–39.

Kitu cha kuburudisha

Changamoto ya Umisionari

Picha
Alt text

Vielelezo na Sammie Francis

Jifunze kuhusu kile wamisionari wanachofanya! Kisha fuata njia na ukabiliane na changamoto.

Wamisionari hukutana na watu na kuzungumza nao.

Pata kumjua mtu katika darasa lako au ujirani wako ambaye humfahamu.

Baadhi ya wamisionari hujifunza lugha mpya.

Jifunze kusema maneno machache kwa lugha nyingine. Unaweza kujifunza kusema, “Yesu ananipenda” au “Mimi ni mwana wa Mungu.”

Wamisionari hushiriki talanta zao! Baadhi hupiga piano kanisani, hujifunza maandiko ya kushiriki au hutumia talanta zingine kwa ajili ya kuwabariki wengine.

Fikiria kuhusu talanta uliyo nayo. Kisha tumia talanta hiyo kumtumikia mtu!

Wamisionari husali kwa ajili ya wengine.

Wafikirie watu wawili au watatu unaowajua na sali kwa ajili yao. Muombe Baba wa Mbinguni awabariki.

Wamisionari huwafunza wengine kuhusu Yesu Kristo.

Mwambie rafiki au mwanafamilia jambo ulilojifunza kuhusu Yesu katika Msingi.

Chapisha