2023
Yesu Alituomba Tushiriki Injili
Julai 2023


“Yesu Alituomba Tushiriki Injili,” Rafiki, Julai 2023, 24–25.

Hadithi za Yesu

Yesu Alituomba Tushiriki Injili

Ondoa ukurasa huu na ukunje katika nusu mbili zinazolingana. Kisha inua picha juu wakati ukisimulia hadithi.

Picha
alt text

Baada ya kufufuka, Yesu aliwatembelea Mitume Wake. Aliwapatia samaki na mkate wale.

Yesu alimwuliza Petero, “Je, wanipenda?”

Petro alisema ndiyo. Kisha Yesu akasema “Lisha kondoo wangu.”

Yesu alimwuliza Petro mara mbili zaidi. “Je, wanipenda?”

Mara zote Petro alisema ndiyo. Na mara zote Yesu alisema, “Lisha kondoo wangu.”

Petro alijifunza kwamba Yesu alikuwa akimwomba ashiriki injili. Yesu ni Mchungaji wetu na sisi ni kondoo Wake.

Tunaweza kuonesha upendo wetu kwa Yesu kwa kuwasaidia wengine wajifunze kuhusu Yeye na wamfuate Yeye.

Chapisha