2023
Nini kiko Akilini Mwako?
Julai 2023


“Nini kiko Akilini Mwako,” Rafiki, Julai. 2023, 42.

Nini kiko Akilini Mwako?

Wazazi wangu hawajaunganishwa hekaluni. Je, hiyo inamaanisha siwezi kuwa sehemu ya familia ya milele?

—Mtu anayejiuliza akiwa Warsaw

Picha
alt text

Mpendwa Unayejiuliza,

Wewe ni mtoto wa wazazi wa mbinguni. Hata kabla hujaja kwenye dunia hii, ulikuwa sehemu ya familia Yao. Na hilo halitabadilika kamwe! Hivyo, lolote liwalo, daima utakuwa sehemu ya familia ya milele!

Baba wa Mbinguni anawapenda sana wewe na familia yako. Anawataka nyote mrejee Kwake. Ataendelea kuwabariki na kuwaongoza wewe na familia yako. Sali Kwake kuhusu wasiwasi wako na Yeye atakufariji.

Kwa upendo,

Gazeti la Rafiki

Mchore kila mmoja wa wanafamilia yako na jambo unalolipenda kuwahusu! Tafuta mema katika familia yako. Waambie kile unachokiona!

Chapisha