2023
Kumfuata Yesu nchini Nepal
Julai 2023


“Kumfuta Yesu nchini Nepal,” Rafiki, Julai 2023, 16–17.

Kumfuata Yesu nchini Nepal

Kutana na Samyog!

Picha
Picha ya mvulana akiwa amevalia kofia

Kuhusu Samyog

Picha
Picha ya mvulana anayetabasamu akiwa ameshikilia mmea ulio ndani ya chungu

Miaka: 9

Kutoka: Jimbo la Bagmati, Nepal

Lugha: Kinepali, Kingereza

Malengo na ndoto: 1) Kuwa rubani. 2) Kumfuata Yesu Kristo. 3) Kumwita mtoto wake wa kwanza wa kiume “Sreejal,” ambayo humaanisha utakaso.

Familia: Samyog, Aama (Mama), Buba (Baba), na didis wawili (dada wakubwa)

Jinsi Samyog Anavyomfuata Yesu

Picha
Picha ya mvulana akicheza kwenye uwanja wa michezo

Nchini Nepal, Wakristo ni wachache. Watu wengi hawafahamu mengi kuhusu Yesu Kristo. Samyog hupenda kuwaambia wengine kuhusu Yesu.

Wakati fulani, shule ya Samyog ilikuwa na sherehe za Krismasi ili kuwasaidia wanafunzi wajifunze kuhusu siku za mapumziko ulimwenguni kote. Samyog alishiriki kwamba yeye ni Mkristo. Alijibu maswali ya walimu na wanafunzi kuhusu Yesu.

“Ninataka kumfuata Yesu maisha yangu yote,” Samyog alisema.

Mambo ayapendayo Samyog

Picha
Sebule, bakuli lenye kuku na kipande cha keki

Hadithi kuhusu Yesu: wakati alipokufa kwa ajili yetu kwa sababu anatupenda

Mahali: Sebule ya nyumbani kwao

Wimbo wa Msingi: “Follow the Prophet” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 110–11)

Vyakula: Keki na kukhura (kuku)

Rangi: Machungwa na samawati

Masomo Shuleni: Sayansi na hisabati

Picha
Alt text

Vielelezo na Aaron Cushley

Chapisha