2023
Ilianzia kwenye Uwanja wa Besiboli
Julai 2023


“Ilianzia kwenye Uwanja wa Besiboli,” Rafiki, Julai 2023, 32.

Rafiki kwa Rafiki

Ilianzia kwenye Uwanja wa Besiboli

Kutoka kwenye mahojiano na Lucy Stevenson Ewell.

Picha
Alt text

Vielelezo na Brian Michael Weaver

Nilipokuwa na umri wa miaka 13, nilicheza kwenye timu ya besiboli pamoja na baadhi ya marafiki. Sikuwa muumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho lakini wawili kati ya wana timu wenzangu walikuwa waumini. Walikuwa mapacha. Majina yao yalikuwa Rob na Lane.

Siku moja tukiwa mazoezini walinialika nije kwenye jioni ya nyumbani pamoja na familia yao. Sikujua jioni ya familia ilikuwa nini, hivyo niliomba ufafanuzi. Waliniambia tungejifunza kuhusu mambo ya kanisa na kuimba nyimbo. Sikuwa na shauku kuhusu hilo. Lakini waliahidi kwamba kungekuwa na kitindamlo, hivyo niliamua kwenda.

Familia yangu ilienda nyumbani kwao kwa ajili ya jioni ya nyumbani. Nilihisi kitu tofauti kabisa. Sikujua ni nini, lakini haikuwa hisia ngeni. Ilikuwa hisia nzuri. Mama yangu aliihisi pia.

Sikujua wakati huo kwamba mama yangu alikuwa muumini wa Kanisa. Alibatizwa wakati alipokuwa msichana. Lakini alikwenda kanisani kwa nadra sana.

Baada ya usiku huo, mama yangu alianza kuhudhuria tena kanisani. Nilikwenda pamoja naye ili nijifunze zaidi. Miezi kadhaa baadaye, nilibatizwa na baba yake Rob na Lane.

Nina shukrani kubwa kwamba Rob na Lane walijali vya kutosha kuhusu mimi kwa kushiriki injili. Leo nimebarikiwa kuwa na familia ya milele. Na hii yote ilianzia kwenye uwanja wa besiboli!

Kama vile Rob na Lane, una ushawishi wenye nguvu sana kwa wengine. Unaweza kuleta tofauti katika familia yako. Unaweza kushiriki injili pamoja na rafiki zako.

Chapisha