2023
Benjamin Anazungumza kuhusu Historia ya Familia
Julai 2023


“Benjamin Anazungumza kuhusu Historia ya Familia,” Rafiki, Julai. 2023, 36–37.

Benjamin Anazungumza kuhusu Historia ya Familia

Benjamin anatokea Buenos Aires, Argentina. Tulimuuliza maswali kadhaa kuhusu historia ya familia.

Picha
Mvulana ameketi na mikono ikiwa imekunjwa

Ni kwa namana gani ulianza kufanya historia ya familia?

Nilianza kufanya historia ya familia nikiwa na baba yangu. Tuliifanya pamoja kila Jumapili. Baba yangu alinisaidia nijifunze jinsi ya kutumia FamilySearch. Ilinibidi niifanyie mazoezi tena na tena. Sasa ninafanya historia ya familia pamoja na baba yangu au binamu yangu Jasmina.

Picha
Mvulana ameketi kwenye kompyuta

Ni kipi unakipenda zaidi kuhusu historia ya familia?

Ninapenda kuwatafuta watu wapya wa kuwaongeza kwenye mti wangu wa familia. Kwanza, ninatafuta kumbukumbu za zamani. Kisha ninatafuta majina ya mababu zangu. Ninatafuta tarehe zao za kuzaliwa na mahali walipozaliwa. Ninatafuta mahala pengine walipoishi pia.

Umejifunza nini kuhusu mababu zako?

Nilijifunza kwamba ninao mababu kutoka Italia na Ujerumani. Mmoja wa mababu zangu kutoka Italia ana jina kama la kaka yangu! Jina la kaka yangu ni “Santiago,” ambayo ni “Giacomo” kwa Kiitaliano. Pia nilijifunza kwamba jina letu la ukoo lilikuwa likitajwa kitofauti.

Picha
Mvulana akiwa ameshikilia ramani ya tufe la ulimwengu

Ni jinsi gani unawasaidia watu wengine kufanya historia ya familia?

Ninamsaidia bibi yangu kutumia FamilySearch. Nilimfunza jinsi ya kuongeza kumbukumbu. Nilimsaidia pia kuwaongeza watu waliokosekana kwenye mti wake wa familia. Baadhi ya jamaa zake walikuwa na majina mengi! Ilichukuwa muda mrefu kuwaweka wote kwenye mti. Lakini nilikuwa na furaha sana kwamba niliweza kumsaidia ajifunze kutumia FamilySearch, kama vile baba yangu alivyonifunza.

Picha
Simu ikiwa na picha ya mvulana anayepunga mkono kwenye skrini

Ni mradi upi wa historia ya familia unataka kuufanya baada ya huu?

Ninataka kutengeneza video kwa ajili ya rafiki zangu na familia yangu ili kuwasaidia wajifunze jinsi ya kutumia FamilySearch. Nilipoanza, ilinibidi nijifunze mengi sana. Ninataka kuwafundisha watu wengine ili waweze kufanya vivyo hivyo.

Picha
PDF ya hadithi

Vielelezo na Laura Zarrin

Chapisha