2023
Kofta kwa ajili ya Mlo wa Mchana
Julai 2023


“Kofta kwa ajili ya Chakula cha Mchana,” Rafiki, Julai 2023, 12–13.

Kofta kwa ajili ya Mlo wa Mchana

“Ni nini hicho cha ajabu unachokula?”

Hadithi hii ilitokea huko Marekani.

Picha
Mvulana akiwa ameketi kwenye meza ya mlo wa mchana

Roy aliketi mezani na kufungua mkoba wake wa mlo wa mchana. Familia yake ilikuwa imehama na hii ilikuwa siku yake ya kwanza kwenye shule yake mpya. Mama yake alikuwa amemwandalia chakula chake pendwa cha Kiarmenia, kofta. Alikuwa na shauku ya kukila!

Roy alifungua karatasi iliyokuwa imezungushwa kwenye kofta. Ilikuwa kama mviringo mrefu, mwembamba wa nyama. Alipenda harufu ya viungo vilivyookwa kwenye nyama. Na shimo katikati liliifanya iwe kama filimbi ndogo. Aliiweka mdomoni na kupuliza. Kisha aling’ata. Tamu sana!

“Hey,” alisema mvulana aliyekuwa kwenye meza iliyo mkabala. “Ni nini hicho cha ajabu unachokula?”

Roy alihisi mashavu yake yakifura. “Ni mlo wangu wa mchana.”

“Vema, hauonekani kuwa mzuri.” Mvulana alicheka.

Roy hakujua nini cha kusema. Hakujua kwamba hakuna mwingine hapa aliyekula kofta. Hakutaka wadhani kwamba alikuwa wa ajabu! Hivyo aliacha mlo wake na kukimbilia nje kwa ajili ya kujificha.

Baada ya shule, Roy alimkuta mama akifungua maboksi.

“Sitaki tena kubeba kofta kwenda nayo shule,” Roy alisema.

“Kwa nini?” Mama aliuliza. “Ni mlo wako uupendao.”

Roy alimsimulia mama kilichotokea shuleni. “Ilikuwa ya kutia aibu!”

“Nasikitika hilo limetokea,” Mama alisema. “Watu wengi hapa hawajawahi kula kofta. Vipi ikiwa tutawapa watoto wengine fursa ya kuionja?”

“Kwa nini?” Roy aliuliza. “Hawataila.”

“Unajua, huwezi kujua mpaka uulize! Najua ni vigumu kupata marafiki wapya. Lakini sisi sote ni watoto wa Mungu. Wakati mwingine yatupasa tu tujue mengi zaidi kuhusu kila mmoja wetu.”

Roy alilifikiria. Hakutaka kuchekwa. Lakini alitaka kuwapa watoto kwenye mlo wa mchana nafasi ya wao kuelewa. Na kofta kweli ilikuwa na ladha nzuri.

Aliitikia kwa kichwa. “SAWA. Acha tutengeneze nyingi zaidi.”

Siku iliyofuata kwenye mlo wa mchana, Roy alivuta pumzi ndefu. Aliketi karibu na mvulana aliyemcheka.

Roy alifungua mkoba wake wa mlo wa mchana. “Kuna yeyote angependa kuonja chakula cha Kiarmenia?”

Watoto wengine walikusanyika wakati Roy akifungua kofta.

“Nitaonja,” mvulana alisema.

“Mimi pia,” msichana aliongeza. Roy alipitisha kofta ili kila mmoja aweze kuonja. Kisha wote waling’ata.

“Hii ni nzuri sana!” mvulana alisema. “kinaitwaje?”

“Kofta,” Roy alisema.

“Vizuri!” Mvulana alitabasamu. “Mimi ni John. Utapenda kucheza wakati wa mapumziko?”

Roy angeweza tu kuitikia kwa kichwa mdomo wake ukiwa umejaa chakula. Mama yake alikuwa sahihi—wao wote walikuwa pia watoto wa Mungu! Na kuwagawia kulimsaidia atengeneze marafiki.

Picha
Alt text

Kielelezo na Mark Robison

Chapisha