2023
Shughuli za Njoo, Unifuate
Julai 2023


“Shughuli za Njoo, Unifuate,” Rafiki, Julai 2023, 6–7.

Shughuli za Njoo UNifuate

Kwa ajili ya jioni ya nyumbani au kujifunza maandiko—au kwa ajili ya burudani tu!

Mfuate Kiongozi

Picha
Alt text

Vielelezo na Katy Dockrill

Kwa ajili ya Matendo ya Mitume 1–5

Hadithi: Baada ya Yesu kufa, Petro aliitwa kuwa kiongozi wa Kanisa la Bwana. Unaweza kusoma hadithi hii kwenye ukurasa wa 46 au Matendo ya Mitume 2–3.

Wimbo: “Stand for the Right” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 159)

Shughuli: Chagua mtu awe kiongozi. Mruhusu kiongozi afanye tendo (kama vile kurukaruka kwa mguu mmoja au kuzunguka). Wengine wanawaiga. Wakati kiongozi anapobadili tendo, wengine wanaiga tendo jipya. Fanya zamu za kuwa kiongozi hadi kila mtu apate zamu.

Msafi tena

Picha
Alt text

Kwa Ajili ya Matendo ya Mitume 6–9

Hadithi: Mtu aitwaye Sauli alijaribu kuharibu Kanisa la Yesu Kristo. Kisha alitubu na kubadili maisha yake. Alikuwa mmisionari na aliwafunza watu kuhusu Yesu Kristo. Alikuja kujulikana kama Paulo. (Ona Matendo ya Mitume 9:1–20.)

Wimbo: “I Know My Father Lives,” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 5)

Shughuli: Shika udongo mikononi mwako. Inakufanya uhisi vipi wakati mikono yako ni michafu? Kisha, osha mikono yako kwa sabuni na maji. Kuosha mikono yetu ni kama kutubu. Kwa sababu ya Yesu, tunaweza kutubu na kuwa safi tena baada ya dhambi.

Changamoto ya Umisionari

Picha
Alt text

Kwa Ajili ya Matendo ya Mitume 10–15

Hadithi: Barnaba na Paulo walikuwa wamisionari (ona Matendo ya Mitume 13:2–4). Waliwafundisha watu kuhusu Mwokozi. Wamisionari leo pia huwafundisha watu kuhusu Mwokozi.

Wimbo: “Tell Me the Stories of Jesus” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 57)

Shughuli: Chagua changamoto kutoka kurasa za 38–39 ili mfanye pamoja, kama vile kumhudumia jirani. Ninaweza kuwa mmisionari sasa.

Picha Yako

Picha
Alt text

Kwa Ajili ya Matendo ya Mitume 16–21

Hadithi: Mtume Paulo alifundisha kwamba sisi sote ni watoto wa Mungu (ona Matendo ya Mitume 17:28–29). Baba wa Mbinguni anawapenda watoto Wake wote. Ametupatia kila mmoja wetu vipawa na talanta tofauti.

Wimbo: “I Am a Child of God” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 2–3)

Shughuli: Chora picha yako. Upande wa juu, andika “mimi ni mtoto wa Mungu.” Kuzunguka picha, andika au chora mambo unayopenda kuyafanya. Ni kwa jinsi gani unaweza kutumia talanta zako kuwasaidia wengine?

Chapisha