2023
Shughuli za Njoo, Unifuate kwa ajili ya Watoto Wadogo
Julai 2023


Shughuli za “Njoo, Unifuate kwa ajili ya Watoto Wadogo,” Rafiki, Julai. 2023, 49.

Agano Jipya

Shughuli za Njoo, Unifuate kwa ajili ya Watoto Wadogo

Picha
Alt text

Kwa ajili ya Matendo ya Mitume 1–5

Wasaidie watoto wako wadogo waseme, “Ninaweza kumfuata nabii.” Waoneshe picha ya Rais Nelson na imba kibwagizo cha wimbo “Follow the Prophet” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 110–11). Zungumzia kuhusu wakati ambapo ulimfuata nabii.

Kwa ajili ya Matendo ya Mitume 6–9

Wakusanye watoto wako wadogo na uzime taa ndani ya chumba. Tumia tochi kuwaongoza kuzunguka chumba. Fafanua kwamba Roho Mtakatifu ni kama tochi kwa sababu Yeye anaweza kutuongoza na kutuonesha njia.

Kwa ajili ya Matendo ya Mitume 10–15

Ukiwa pamoja na watoto wako wadogo, tazama picha za watoto wenye rangi tofauti za ngozi, aina za mwili na uwezo wa kimwili. Fafanua kwamba Baba wa Mbinguni anawapenda watoto Wake wote. Wasaidie watoto wako wadogo watengeneze moyo kwa mikono yao na waushikilie karibu na picha.

Kwa ajili ya Matendo ya Mitume 16–21

Wasaidie watoto wako wadogo watengeneze beji za umisionari zikiwa na majina yao kamili na jina kamili la Kanisa. Fafanua kwamba Wamisionari hufundisha watu kuhusu Yesu. Gundisha beji na wasaidie watoto wako wadogo waseme kwa nini wanampenda Yesu.

Chapisha