“Salamu kutoka Nepal!” Rafiki, Jul. 2023, 18–19.
Salamu kutoka Nepal!
Jifunze kuhusu watoto wa Baba wa Mbinguni ulimwenguni kote.
Nepal ni nchi iliyo Kusini mwa bara la Asia. Takribani watu milioni 30 wanaishi huko.
Bendera Maalumu
Nepal ndiyo nchi pekee yenye bendera isiyo na umbo la mstatili! Ina jua na mwezi juu yake.
Mlima Evarest
Nepal ni makazi ya mlima mrefu zaidi ulimwenguni, ambao una urefu wa futi 29,032 (8,849 m). Zaidi ya watu 6,000 wameupanda mpaka kileleni.
Marafiki wa Kihindu
Watu wengi wa Nepal wanafuata dini ya Hindu. Katika dini hii, ng’ome ni wanyama watakatifu ambao hutendewa kwa heshima.
Dal Bhat
Kila siku watu hula mlo wenye dal (dengu) na bhat (wali). Mara nyingi hula vyakula vingine pamoja na chakula hicho, kama vile mchanganyiko wa mboga zenye pilipili na mboga zilizochachushwa.
Kitabu cha Mormoni
Kitabu kizima cha Mormoni kilichapishwa katika lugha ya Nepali kwa mara ya kwanza mnamo 2017. Waumini wa Kanisa huko walikuwa na furaha sana!