2017
Andrea na Neno Baya
April 2017


Andrea na Neno Baya

Mwandishi anaishi Utah, Marekani.

“I’ll try to repent, to do better, to pray” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 98).

Andrei and the Bad Word

Unafikiri wewe ni bora zaidi kuliko mtu mwingine ye yote kwa sababu wewe huapi, Nikolai alisema wakati wa mapumziko.

“Hiyo siyo kweli,” alisema Andrea.

“Kwa hiyo kwa nini husemi neno moja la kuapa? Moja tuu? Halitakuua. Kila mtu anaapa.”

Andrea alipandisha mabega. “Sitaki tuu kufanya hivyo.”

Andrea alijua kuapa kulikuwa ni makosa na kunamfanya Roho Mtakatifu aondoke. Andrea alimtaka Roho Mtakatifu awe pamoja naye. Kwa hiyo hakuapa.

Andrea alikuwa mgeni shuleni, na kwa kadri ilivyokuwa, Nikolai alikuwa mtu pekee katika darasa lake la sita aliyetaka kuwa rafiki yake. Lakini Nikolai alimsumbua kuhusu kuapa kila siku ipitayo. Na kila siku Andrea alikuwa anachoka zaidi kusema hapana. Aidha, Andrea aliogopa kwamba Nikolai angeacha kuwa rafiki yake, na kisha kwa kweli atakuwa mpweke.

“Sema tuu neno moja la kuapa,” Nikolai alisema baada ya shule. “Kisha nitakuacha sitakusumbua tena.”

Mwishowe Andrea alichoka sana kusumbuliwa kwamba aseme neno moja la kiapo—moja ambalo halikuwa baya sana.

Nikolai alikubali kwa kichwa. “Vizuri, sasa wewe ni mmoja wetu.”

Baada ya hapo, marafiki wengine wa Nikolai walizungumza na Andrea pia. Walikula chakula cha mchana pamoja naye na walicheza mpira wa miguu pamoja naye wakati wa mapumziko. Lakini kuwa katika kundi la marafiki wa Nikolai ilikuwa kama kutembea kwenye tetemeko la ardhi. Kadiri Andrea alivyozidi kuishi pamoja nao, ndivyo alivyozungumza zaidi na kufanya kama wao. Na wote waliapa. Sana. Walichekana na kutukanana. Walisema mambo yasiyo na adabu kuhusu walimu wao. Walishikwa na wazimu na kufanya mambo mengi ya aibu. Pole pole Andrea alianza kusikia hasira mara kwa mara na kupata zaidi na zaidi sababu za kuapa.

Siku moja usiku wakati mama na baba wametoka, Andrea na dada yake mkubwa Katya walianza kubishana kuhusu maonesho gani ya kuangalia. Kabla Andrei bado hajafikiria kuhusu hilo, neno la kiapo liliruka mdomoni mwake.

Katya aliangalia kwa mshangao. “Ninamwambia Mama.”

Andrea alikimbilia kwenye chumba chake cha kulala na kufunga mlango kwa nguvu. Kosa lilikuwa nini kwa kila mmoja? Kwa nini wao walikuwa wanamfaya yeye kuwa mwenda wazimu wakati wote? Wazazi wake waliporudi nyumbani, Andrea alifungua mlango wake kidogo na kumsikia Katya akisema, “Mama, Andrea aliniapia.”

“Nini?” Mama alisikika kuwa ameshangazwa. “Andrea kamwe hawezi kuapa.”

Andrea alifunga mlango na kujibwaga kwenye kitanda chake. Alijifikiria jinsi alivyokuwa tofauti tangu alipoanza kuapa. Imekuwa ni muda mrefu tangu alipojisikia kuwa alikuwa na Roho Mtakatifu.

Andrea alipiga magoti pembeni mwa kitanda chake na kuomba. “Mpendwa Baba wa Mbinguni, nasikitika nimekuwa ovyo na mwenye hasira. Ninasikitika nilianza kuapa. Ninakwenda kufanya vizuri zaidi.”

Wakati Andrea alipokuwa anaomba, hisia nzuri zilijaza moyo wake. Kwa mara ya kwanza tangu alipoanza kuapa, alisika furaha ya kweli. Alijua Mungu alimpenda, na aliweza kumhisi Roho Mtakatifu. Alijisikia kusamehewa na alijua angeweza kubadilika na kuwa mwema zaidi.

Baada ya maombi yake, alimwambia Mama ukweli na alimwomba radhi Katya. Andrei alijisikia vizuri zaidi baada ya hapo. Nilijisikia vizuri kutubu.

Siku ya pili shuleni, Andrea hakula chakula cha mchana pamoja na kundi la Nikolai. Badala yake alikaa karibu na baadhi ya watoto asiowajua. Itachukua muda, lakini Andrea alijua atawapata marafiki waliokuwa wazuri na wenye furaha na wasioapa. Kama vile yeye.