Ufanye Ujumbe kuwa Wako katika Kujijifunza Kwako Injili
Angalia dokezo hizi za kujifunza injili na kutafuta majibu kwa maswali ya kiroho.
Ni jinsi gani unasoma wakati unapotafuta majibu ya swali la kiroho au hata unapojaribu tu kuelewa maandiko vizuri zaidi? Ninamaanisha wewe—binafsi. Kila mtu ana tabia tofauti za kujifunza kwa ajili ya shule, lakini mara nyingine sisi husahau ya kwamba tunaweza kuufanya ujumbe kuwa wetu binafsi katika kusoma kwetu injili pia. Wakati utakapokuwa na swali la kiroho au la kimafundisho, jaribu baadhi ya vidokezi hivi ili kugundua ni kipi kitakuwa bora zaidi kwako.
1. Tengeneza
Tengeneza orodha, chati, au ramani. (Tazama mfano hapa chini.)
Tengeneza mtandao wa kusoma. Andika maneno na mawazo na kisha uyaunganishe na laini na viputo kuonyesha jinsi yanavyohusiana.
2. Andika
Andika mawazo na hisia unazopata wakati unaposoma maandiko katika shajara ya kujifunzia kusoma na ufanye mapitio ya mawazo hayo mara kwa mara.
Andika chini mawazo na hisia zako baada ya maombi yako, hata kama hisia hizo hazihusiani moja kwa moja na mada unayosoma. Ona kile ambacho Roho anakufundisha baada ya muda.
Andika maswali yako katika daftari, kwenye simu yako, au kijitabu kilicho kando ya kitanda chako kukukumbusha na kukusaidia kuendelea kufikiria kuhusu yale unayojifunza kila siku.
3. Sikiliza na Ujadili
Zungumza na mzazi au kiongozi anayeaminika. Ifanyieni kazi kwa pamoja. Yaweza chukua muda mrefu, lakini nyote wawili mtakua katika mchakato huo.
Mfundishe Mtu Mwingine. Chukueni zamu kushirikiana kile mnacho fahamu. Jadilianeni kile mlichojifunza kutoka kwa kila mmoja.
Sikilizeni maandiko au simulizi zingine na vyanzo vingne vya WSM kwa sauti.
4. Uchunguzi
Chunguza misaada mingine ya kujifunza iliyoko katika maandiko na kwenye mtandao (tazama hapa chini ili kupata orodha ya nyenzo za usaidizi za WSM).
Chunguza kwenye LDS.org upate video na nyimbo kuhusu unacho jifunza.
Soma muktadha. Chunguza historia au sura zinazozingira mada au maandiko unayosoma.
5. Fanya
Igizeni simulizi kutoka kwenye maandiko au nyenzo zingine. Ni jinsi gani kuvaa viatu vya mtu yule yaweza kukusaidia kuelewa vyema kile unachosoma? Ni jinsi gani hali kama hizo zingeonekana katika maisha yako?
Tengeneza mtiririko wa maandiko ambao unaunganisha majibu unayopata katika maandiko yako. (Tazama mfano hapa chini.)