Nafasi Yetu
Mungu Hutupa Sisi Zana
Mjomba wangu ni msanii na anatengeneza meli ndogo ndogo za mbao katika chupa za kioo. “Inachukua muda mrefu, umakini, na juhudi kuzitengeneza.
Siku moja niliona zana zake zote na kuona jinsi kila zana inavyotumika kwa kazi maalumu au kunakshi juu ya meli. Nilipo mwangalia akifanya kazi, nilishangazwa kwa jinsi alivyotumia zana hizo ili kutengeneza meli hizi. Nilikumbushwa hadithi ya Nefi akijenga meli (ona 1 Nefi 17–18). Aliijenga kulingana na njia ya Bwana, sio njia ya binadamu. Mungu hutupa zana ili kujenga meli zetu wenyewe kwa njia Yake. Maandiko, imani, na upendo wa Mungu ni zana ambazo lazima nizitumie katika maisha yangu mwenyewe ili kwa uangalifu nijenge meli yangu mwenyewe pasipo kuweka nyufa. Najifunza kila siku kuwa mwanafunzi wa Bwana.
Maria Mercedes G. Monagas, Venezuela
Kujisikia Mpweke
Ilikuwa majira ya a kuchipua ya baridi nchini Denmark. Ndio kwanza nimeanza umisionari, na ushuhuda wangu ulikuwa wa kuhangaika sana. Nilikuwa mwongofu wa miezi 19 tu na mwenye mashaka kuhusu kukabiliana na nchi ngeni, lugha nisiyoweza kuisema, na mzingile wa mitaa nisioweza kuelewa jinsi ya kujiongoza. Maombi yangu ya mwanzo yaliyojaa shukrani mara yakawa mashitaka makali: “Mungu, kwa nini umeniacha mpweke?”
Asubuhi moja nilimsihii Yeye katika maombi. Lakini badala ya kumuuliza “kwa nini” huku nikiwa na hasira katika moyo wangu, niliomba ushahidi wa ukweli wa injili na ukomeshaji wa mashaka yangu.
Baada ya kuomba,nilifunua maandiko yangu. Nilitua kwenye Kumbu kumbu la Torati 31:6: “Iweni hodari na moyo wa ushujaa, msiogope wala msiwahofu; kwa maana Bwana, Mungu wako, yeye ndie anayekwenda pamoja nawe hatakupungukia wala kukuacha.”
Roho yangu ilijaa furaha nilipotambua jibu kwa maombi yangu: Mungu amekuwa pale wakati wote. Alikuwa tu anangojea maombi yangu ya dhati kuliko mashitaka ya kuachwa.
Mungu kamwe hataniacha, hata wakati mambo yote yanaonekana hayafai. Na tunaweza kuhisi mwanga Wake wa jua kwa njia ya maombi na maandiko Yake.
Clayton E. Texas, Merokani