Sauti za Watakatifu wa Siku za Mwisho
Tayari!
Wakati wa usahili wangu kama askofu Jumapili moja jioni, nilipata nafasi ya kukaa chini pamoja na rafiki yangu mzuri kuongea kuhusu baadhi ya changamoto alizokuwa anakabiliana nazo. Baada ya kusikiliza matatizo yake kwa dakika chache, nilihisi kwamba alichokuwa anahitaji ni kusoma maandiko mara kwa mara. Pia nilikumbushwa kwamba, kama askofu wake, na mimi pia natakiwa kusoma maandiko mara kwa mara, kitu ambacho nilikuwa nasumbuka nacho. Hivyo nilipendekeza kwamba tuwe “washirika wawajibikaji” katika kujitahidi kujifunza kwa mfululizo zaidi.
Kila siku baada ya kumaliza kusoma maandiko, tulitumiana ujumbe mfupi wa neno Tayari! Tukijua kwamba kuna mtu mwingine alikuwa anasubiri kusikia iwapo amemaliza au hajamaliza kusoma kwa siku ile ilikuwa ni kuhamasishana kwetu wote. Kama mmoja wetu amesahau, kupata ujumbe mfupi ilikuwa ni kukumbushwa. Kama mmoja wapo hajatuma ujumbe mfupi, hakuachwa nyuma Tuliacha kila mmoja wetu achukue changamoto hii bila ya kumfanya mwingine ajisikie vibaya.
Tuliianzisha changamoto hii miezi sita iliyopita sasa, na sikumbuki siku ambayo tulikosa kusoma maandiko yetu. Kaka huyu alisimama wakati wa kipindi cha mfungo na ushuhuda miezi mwili iliyopita na kutoa ushuhuda wake wa matokeo mazuri aliyo yapata akiwa anasoma maandiko kila siku yeye na familia yake.
Ninamshukuru kaka huyu na urafiki wake, na pia ujumbe wake mfupi wa kila siku. Nimeona jinsi tekinolojia, inapotumika vizuri, inavyoweza kuendeleza maisha yetu. Pia ninashukuru kwa ajili ya maandiko na jinsi yanavyo shuhudia juu ya Kristo. Ninajua kwamba dhabihu ya kulipia dhambi ya Mwokozi inamwezesha kila mmoja wetu kurudi kuishi pamoja Naye siku moja.