2017
Ninawezaje kujua kama Mungu anasikiliza maombi yangu?
April 2017


Maswali & Majibu

“Ninawezaje kujua kama Mungu anasikiliza maombi yangu?”

Maombi ni baraka kubwa, na tumeahidiwa kwamba Baba wa Mbinguni kila mara anasikiliza, lakini mara nyingi inakuwa kazi kutambua majibu Yake.1

Fikiria juu ya hili: ama Mungu anakusikiliza wewe au Hakusikilizi. Kama hakusikilizi, hivyo basi hakuna sababu ya kuomba. Lakini kama ndiyo (na Anafanya!), inabidi tuelewe ni jinsi gani hakika tunawasiliana Naye kwa maombi, tambua majibu, na kwa uaminifu songa mbele.

Tunapohisi Yeye hasikilizi, huenda sisi tunahitaji uzoefu wa kukua binafsi. Unaweza kujiuliza wewe mwenyewe maswali machache: Je, mimi ni msafi? Je, malengo yangu ni yenye kustahili? Je, niko tayari kutenda yale anayoniambia?2 Kama jibu kwa kila swali ni ndio, unaweza kuamini kwamba “Bwana Mungu wako … atakupa majibu ya maombi yako” (M&M 112:10). Kumbuka, wakati mwingine majibu huja katika njia ya kutatiza au isiyo tarajiwa.

Kama ulijibiwa hapana kwa baadhi ya yale maswali, bado hujachelewa! Fanya masahihisho ya lazima katika maisha yako ili uweze kuwa na Roho. Kubali kufuata miongozo unayopokea.

Na usisahau kwamba kila mtu anapokea majibu kwa njia tofauti. Omba kwamba Roho Mtakatifu akufundishe wewe jinsi wewe unavyoweza kutambua majibu. Huenda isiwe rahisi kuyatambua kwa mara ya kwanza, lakini ni sawa na ujuzi mwingine: mazoezi hufanya mazoea. Kuwa na imani na amini kwamba Baba wa Mbinguni ana sikiliza wakati wote.

Msikilize Roho

Jaribu kumsikiliza Roho Mtakatifu. Watu humsikiliza Roho Mtakatifu kwa njia tofauti, hivyo huenda unasikiliza sauti, ndogo tulivu wakati yawezekana mwongozo unakuja kama hisia. Ninajua kwamba Roho Mtakatifu atakuambia wewe yale yote unayohitaji kujua—unatakiwa kusikiliza tu.

Elise G., umri miaka 13, Alberta, Canada

Majibu katika Kanisa

Mara moja nilipata kuwa na wasiwasi mkubwa kuhusu kwenda miadi pamoja na mtu asiye muumini. Jumapili moja katika kipindi cha sakramenti, dada mmoja alitoa hotuba ambayo ilionekana kunilenga mimi moja kwa moja. Kwa wakati huo, nilipokea uhakikisho kwamba Bwana amejibu maombi yangu. Kabla, nilikuwa nimechanganyikiwa kuhusu nini nifanye, lakini wakati huo nikafarijiwa na Roho Mtakatifu, ambaye aliujaza moyo wangu kwa furaha na ujasiri. Mungu anatujibu sisi kupitia hisia, mawazo, maandiko, na hata wazungumzaji kanisani!

Karen V., umri miaka 19, Minas Gerais, Brazili

Tafuta

Wakati fulani nilijiuliza kama Mungu angeweza kusikia maombi yangu, na kisha nikahisi jibu katika moyo wangu. Nilimsikia mtu akitoa ushuhuda kuhusu maombi, nami nilihisi Roho Mtakatifu. Ushauri wangu mwingine utakuwa ni kuwauliza wazazi wako, askofu, au waumini wengine wa kata yako. Unaweza hata kuomba kwa ajili ya msaada kwenye mada hii!

Joshua S., miaka 13, Oregon, USA

Kumbuka Wewe Ni Nani

Ninajua Mungu anatusikiliza sisi kwa sababu maombi hutoa hisia za amani, faraja, na upendo katika moyo wangu. Ninaona kwamba Yeye ameniepusha na hatari nyingi siku hadi siku kwamba anailinda familia yangu, na nahisi kupendwa na Yeye. Kabla sijaenda shuleni, mara nyingi ninasema kauli mbiu ya Wasichana; inanisaidia mimi kukumbuka kwamba mimi ni binti wa Baba wa Mbinguni, ambaye ananipenda.

Nicol M, umri miaka 19, Lima, Peru

Maombi ya Mtoto

Ninajua Baba wa Mbinguni anayasikia maombi yangu kwa sababu ya maneno haya katika wimbo wa Watoto “A Child’s Prayer” (katika Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 12): “Heavenly Father, are you really there? Na je unasikia na kujibu kila ombi la mtoto? Baadhi wanasema kwamba mbingu ipo mbali, lakini nahisi iko karibu nami wakati ninapoomba.” Wakati ninapoukumbuka wimbo huo, ninajua Yeye anasikiliza kwa sababu ninamhisi Roho Mtakatifu na upendo Wake usio na mwisho kwangu. Ninapokumbuka kwamba Yeye ananipenda, ninaona faraja na kujua kwamba anayasikia maombi yangu.

Elaine B., umri miaka 16, Carolina Kaskazini, Marekani

Mwamini Yeye

Baba wa Mbinguni mara zote anayasikiliza maombi yetu, lakini wakati mwingine inaonekana kama hajibu maombi yetu kwa sababu huenda asijibu jinsi au wakati tunamtaka Yeye ajibu. Tunahitaji kuwa tayari kuyaweka mapenzi yetu Kwake na kuwa na imani kwamba Yeye anajua kilnachotufaa sisi. Baba wa Mbinguni anatupenda na mara zote anajaribu kutusaidia kujifunza na kukua akiwa anajibu maombi yetu.

Mosia M., miaka 17, Utah, Marekani

Ombeni Nanyi Mtapewa

Kupitia maandiko, tunafundishwa kwamba Mungu wakati wote atayasikia maombi yetu na atayajibu kama tunawasiliana Naye kwa imani na kwa nia ya dhati. Katika mioyo yetu tutahisi uthibitisho kwamba Yeye anatusikia, hisia za amani na tulivu. Pia tunaweza kuhisi kwamba kila kitu kitakuwa sawa kama tunafuata mapenzi ya Baba. Kama tunatia shaka kwamba Yeye anatusikia sisi, tunahitaji kutafuta mwongozo katika maandiko na kisha tunaomba kujua kama mambo yale tunayosoma ni ya kweli.

Constanza L., umri miaka 20, Bío Bío, Chile

Omba kwa Uaminifu

Baada ya maombi yako, unaweza kusikiliza hisia na dhamira ambayo inakuja kwenye moyo wako. Moja wapo linaweza kuwa jibu la maombi yako. Wakati tunapoomba kwa dhati na moyo wa uaminifu, Baba yetu wa Mbinguni anajibu kulingana na imani tuliyo nayo Kwake. Hajibu tu kwa ajili ya kuridhisha udadisi wetu.

Jean-Claude N., miaka 16, Kasaï-Kati, Jamhuri ya Kidemocrasia ya Kongo