2017
Tafadhali Usiucheze Wimbo Huo
April 2017


Sauti za Watakatifu wa Siku za Mwisho

Tafadhali Usiucheze Wimbo Huo

children listening to sterio

Vielelezo na Bradley H. Clark

Muda fulani uliopita, familia yangu na mimi tuliishi Veracruz, Mexico, ambako watoto wangu walihudhuria shule ya msingi. Kila asubuhi nilipokuwa nawasaidia watoto wangu watatu kuwa tayari kwenda shule, tulisikiliza radio—kituo kilichopendwa sana jijini—na mfuatano wa vipindi uliofurahisha sana ulioongozwa na kijana wa kiume mtangazaji wa radio.

Tulianza kusikiliza wimbo wa kuvutia sana. Nilipoanza kusikiliza kwa makini maneno ya wimbo, nilitambua kwamba mambo yaliyokuwa yanasemwa, ingawa sio ya kishenzi, yalikuwa yenye kushawshi mabaya na yasiyo na maadili.

Nilisema kwa kudhamiria kwa watoto wangu, “Hatuwezi kusikiliza aina hii ya lugha.” Labda hawakusikiliza hata kidogo maneno ya wimbo wenyewe, lakini walisikiliza vya kutosha kuweza kuimba tuni yake huku mdomo ukiwa umefungwa.

Waliniona nikizima sauti ya redio hiyo na wakaniuliza nilikuwa nafanya nini. “Ninakwenda kumwambia mtangazaji wa radio hii kuuondoa wimbo huo kutoka kwenye programu.” Mshangao wao ulinitia moyo kuchukua hatua zaidi.

Hawakuweza kuamini na hata mimi sikuweza kuamini, lakini niliinua simu na kukipigia kituo cha radio. Sikutegemea kupata jibu, lakini kwa mshangao wangu, mtangazaji yule yule wa radio tuliyemsikia kwenye burudani alijibu simu yangu mara moja.

Nilimwambia kwamba sikukubaliana na kusikilizwa kwa wimbo ule, kwa vile familia nyingi ilikuwa imetuni radio yao wakati ule asubuhi. Yeye aliniuliza ningepedekeza aubadilishe na nini, lakini mwenendo wake ulikuwa wenye adabu nzuri kiasi kwamba nilimwomba tu asiucheze wimbo huo wakati wa muda ambao watoto wapo nyumbani.

Sikugundua kama simu yangu ilikuwa hewani, lakini nilikuwa nimeshukuru tu kwamba mtagazaji yule wa radio amesikiliza. Na kwa siku chache zilizofuata, niliweza kusema kwamba ombi langu limekubaliwa.

Tukio lile limenihakikishia kwamba tunapaswa kuwa na ujasiri wakati inapokuwa mikononi mwetu kufanya maamuzi na kufanya kilicho cha muhimu ili kuwalinda watoto wetu kutokana na vishawishi hasi. Tunapofanya hivyo, Roho Mtakatifu anaweza kuendelea kuwa mwenza wetu wakati wote.