2017
Kuokolewa Ukumbini
April 2017


Sauti za Watakatifu wa Siku za Mwisho

Kuokolewa Ukumbini

mother with children in the foyer

Kielelezo na Allen Garns

Mume wangu mara nyingi alitakiwa kufanya kazi Jumapili, akiniacha mimi kuwa msimamizi wa watoto wetu wakiume wanne kanisani peke yangu. Jumapili moja ya kukumbukwa wakati wa kipindi cha sakramenti, watoto wangu wawili walikuwa wakigombana. Kama nikimfanya mmoja wa wavulana hawa kukipenda kitabu, kaka yake atakitaka. Nilijaribu vitafunwa, wanasesere, na kupaka rangi, lakini hakuna kilicho fanya kazi. Nilikuwa nimeshindwa kwa watoto wangu, ambao hawakuonekana kuwa wangekaa chini kimya kwa saa moja.

Nikatoa kitu kidogo cha kuchezea kwenye mkoba wangu na kumpa mtoto wangu wa mwaka mmoja. Mara moja kilio cha nguvu kilikuja kutoka kwa mwanangu wa- miaka- mitatu, Tyson wakati alipomvamia kaka yake mdogo, akijaribu kumpokonya mwanasesere. Niliaibika nikiwa nimewabeba watoto wawili waliokuwa wakipiga kelele na kugombana kwenda nje ukumbini.

Uso wangu ghafla ulilowa kwa machozi ya moto. Kwa nini hili linakuwa gumu? Nilikuwa nafanya kile ambacho Baba wa Mbinguni alitaka mimi nifanye kwa kuileta familia yangu kanisani, sawa? Lakini nisingeweza kufanya tena. Nilikuwa nimechoka na kuaibika kwa kugombana kwa watoto wangu katika kipindi cha sakramenti peke yangu kila wiki. Sikutaka kurudi tena.

Nilikaa na mawazo haya kwa sekunde 15 tu, kisha dada ambaye sikumfahamu vizuri akatoka nje ukumbini kunifuata. Jina lake lilikuwa Dada Beus. Mara nyingi alikaa peke yake, huku mume wake akihudumu katika uaskofu na watoto wake walikuwa wakubwa. Alisema, “Mara zote uko hapa peke yako! Ninaweza kuona kwamba unajitahidi sana. Je, Tyson anaweza kukaa na mimi?” Sikuweza kufikiria jibu! Nilikubali kwa kichwa akiwa anamchukua kwa mkono na kumwongoza, sasa akiwa mtulivu na mwenye furaha, akirudi kanisani.

Nikafuta machozi yangu, nikamchukua mtoto wangu, na kwa unyenyekevu kurudi tena kanisani kufurahia mkutano kwa amani.

Jumapili iliyofuata tukiwa tunaingia katika mkutano wa sakramenti, Tyson alimtafuta rafiki yake mpya. Usiku angeomba, “Asante, Baba wa Mbinguni, kwa ajili ya Dada Beus. Ninampenda sana!”

Imekuwa miaka mitatu, na Tyson bado anamtafuta Dada Beus kanisani. Mwaka uliopita aliitwa kuwa mwalimu wa Watoto wa Msingi darasa la Tyson. Alikuwa mvulana mdogo mwenye furaha aliye hai.

Ninafuraha tele kwa Dada Beus na kukubali kwake kuwapenda na kuwatumikia wengine. Ninajua kwamba tunaweza kubariki maisha ya wengine wakati tunapohudumu kama Mwokozi alivyofanya.