2017
Kufufuka kwa Yesu Kristo na kweli kuhusu Mwili
April 2017


Kufufuka kwa Yesu Kristo na kweli kuhusu Mwili

Kupitia Ufufuko Wake, Yesu Kristo alitufundisha kweli muhimu kuhusu Mwili.

Picha
Resurrected Christ with Thomas

Maelezo ya kina kutoka The Doubtiful Thomas, na Carl Heinrich Block

Background O janniwet/istock/Getty Images

“Alisema, Imekwisha: Akainama kichwa, akaisalimu roho yake” (Yohana 19:30). Wakati ule, roho ya Yesu Kristo iliuacha mwili wake—mwili ambao umevumilia mateso ili kwamba aweze kulipia dhambi za watu wote na kuwasaidia katika udhaifu wao (ona Alma 7:12–13). Mwili ule, sasa ambao ni chombo kitupu, ulitolewa kutoka msalabani, ukaviringishwa katika nguo za kitani, na hatimaye kuwekwa katika kaburi. Siku ya tatu, wanawake wakilikaribia kaburi walikuwa pale ili kukamilisha matayarisho ya maziko kwa ajili ya mwili ule.

Lakini mwili ulikuwa umetoweka.

Ugunduzi wa kaburi tupu ulikuwa ndio mwanzo tu. Mariamu Magdalena, Mitume, na wengine wengi baadaye walishuhudia kitu cha kimiujiza: Yesu Kristo mfufuka, mkamilifu, katika umbo la kibinadamu lenye kugusika.

Mwokozi alihakikisha kwamba wale walio mshuhudia baada ya kufufuka kwake walielewa kikamilifu aina gani ya mwili aliokuwa nao. Aliwaalika Mitume, kwa mfano, kuushika mwili Wake ili kwamba waweze kujihakikishia wenyewe kwamba Yeye alikuwa na mwili halisi na sio roho (ona Luka 24:36–40).1 Hata alikula pamoja nao (ona Luka 24:42–43).

Wakati Mitume wakiwa wanatimiza amri waliyopewa ya kuhubiri injili ya Yesu Kristo, walikabiliwa na upinzani na mateso, baadhi ya hayo yalikuja kwa sababu wao walifundisha kwamba Yesu Kristo alifufuka na kwamba binadamu wote wangefufuka kama matokeo ya hilo (ona Matendo 4:1–3).

Leo, Ufufuko wa Yesu Kristo ni kitovu cha ujumbe unaotangazwa kwa ulimwengu na Kanisa Lake kama ilivyokuwa wakati ule. Kama Nabii Joseph Smith Alivyosema: “Kanuni za msingi za dini yetu ni ushuhuda wa Mitume na Manabii, kuhusu Yesu Kristo, kwamba alikufa, akazikwa, na akafufuka tena siku ya tatu, na kupaa mbinguni; na mambo yote mengine ambayo yanahusiana na dini yetu ni viambatisho tu”2

Ufufuko unasaidia kujibu maswali ya msingi kuhusu asili ya Mungu, asili yetu na uhusiano wetu na Mungu, makusudi ya maisha haya, na matumaini tuliyo nayo katika Yesu Kristo. Hapa pana kweli chache zilizo sisitizwa na ufufuko wa Yesu Kristo.

Baba wa Mbinguni Ana Mwili Uliotukuka

Picha
First Vision

The First Vision, by Gary L. Kapp

Wazo la kwamba Mungu ana umbile la binadamu kwa hakika limeota mizizi katika Biblia,3 vilevile katika fikra zinazopendwa, lakini desturi nyingi za kiteolojia na falsafa za kidini zimeikataa na kupendelea Mungu “asiye na mwili, sehemu, au hisia kali,”4 tangu wakati ule, kwa mtazamo huu, mwili (na maada kwa kawaida) ni uovu au sio ya kweli, kwa maana hiyo roho, akili, au mawazo ni kitu chenye kweli ya msingi na hatima ya kuwa au ni kitu halisi.

Jinsi gani kupendeza kwa kawaida na kimapinduzi, ulikuwa, ufunuo huu wa asili ya Mungu kupitia Mwanawe, Yesu Kristo.

Wakati wa huduma yake, Mwokozi alisema, “Aliyeniona mimi amemwona Baba” (Yohana 14:9). Hii ilikuwa kweli zaidi baada ya Ufufuko Wake na mwili mkamilifu, mwili usiokufa, ambao ulionesha kwamba “Baba ana mwili wa nyama na mifupa unao shikika kama wa binadamu; na Mwana pia” (M&M 130:22).

Asili ya mwili wa Baba wa Mbinguni ndivyo ilivyo funuliwa. Kama Joseph Smith alivyoeleza baadaye, “Kile ambacho hakina mwili au sehemu sio kitu. Hakuna Mungu mwingine ndani ya mbingu lakini Mungu yule aliye na nyama na mifupa.”5

Mzee Jeffrey R. Holland wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili ameiweka katika njia hii: “Kama kuwa na mwili sio tu hakuhitajiki lakini haipendezi kwa Mungu, kwa nini Mkombozi wa wanadamu aliukomboa mwili Wake, akiukomboa kutokana na kushikwa na mauti na kaburi, kuuhakikishia kamwe hautatengana tena na roho Yake kwa sasa au milele? Yo yote ambaye ana puuza dhana ya Mungu mwenye mwili anapuuza vyote Kristo aliyekuwa na mwili wenye kufa na Kristo mfufuka.”6

Baba wa Mbinguni ni mwenye Nguvu- Zote, Mjua -Yote, Upendo- Wote

Sifa bora kabisa za tabia ya Baba wa Mbinguni zimefunuliwa pia katika tendo halisi la ufufuko wa Yesu Kristo. Kama Mzee D. Todd Christofferson wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alivyosema, “Kutokana na ukweli wa Ufufuko wa Kristo, mashaka kuhusu kudura, kujua yote, na ukarimu wa Mungu Baba—aliyemtoa Mwanae wa Pekee kwa ajili ya ukombozi wa ulimwengu—mashaka haya hayana msingi.”7

Uwezo, maarifa, na uzuri wa Mungu vimethibitishwa kwa Ufufuko wa Yesu Kristo. ambao unatoa ushahidi wa hekima na upendo katika mpango wa Baba wa Mbinguni na uwezo wa (Mwanawe) wa kufanya hilo.

Sisi ni watoto wa Mungu

Kama Biblia inavyo tufundisha, tumeumbwa kwa mfano wa Mungu wanaume na wanawake:’ (Mwanzo 1:27) Ufufuko wa Yesu Kristo uliuongezea nguvu ukweli huu. Ukweli ni kwamba, katika saa ile ile ya Kufufuka kwake, Yesu Kristo alisisitiza uhusiano wetu kwa Baba wa Mbinguni, akisema, “Napaa kwenda kwa Baba yangu, naye ni Baba yenu; na kwa Mungu wangu, naye ni Mungu wenu” (Yohana 20:17; mkazo umeongezwa)

Mwokozi alifunua kwamba Mungu na mwanadamu sio kabisa hawafanani kati yao katika kuwepo kwao kiasili. Umbile la msingi la miili yetu ni sawa na lile la roho zetu,8 na roho zetu ziliumbwa kwa mfano wa Mungu kwa sababu hiyo ndiyo asili ya uhusiano kati ya mzazi na mtoto.

Mwili ni kipawa cha Kuwezesha na cha Kuadilisha

Picha
sleeping infant

Picha na David Stoker

Kupitia Ufufuko Wake, Mwokozi alituonesha sisi kwamba mwili, uliopo kwa kuunganishwa ni sehemu muhimu ya kuwepo kwa Mungu milele na watoto Wake. Kama Bwana alivyo mwonyesha Joseph Smith, Vitu vya asili ni vya milele, na roho na vitu vya asili, ambavyo vimeungana na haviwezi kutenganishwa, hupokea shangwe kamilifu (M&M 93:33). Huku kuunganishwa kusikoweza tenganishwa kunaunganisha roho na maada za kimwili pamoja na hivyo vinakuwa kimoja kisicho kufa, kisicho haribika, kitukufu, na mwili kamili—aina pekee ya mwili wenye uwezo wa kupokea ukamilifu wa furaha ambao Mungu anao.

Kinyume na hayo, baada ya kuwa na maumbile ya kimwili na kisha kutenganishwa nayo na kuingia ulimwengu wa kiroho, wafu [wanaona] juu ya kutokuwepo kwa roho zao kutoka kwenye miili yao kama kifungo (M&M 138:50; ona pia M&M 45:17).

Hata miili yetu yenye kufa ni sehemu muhimu ya mpango wa Baba wa Mbinguni na sisi ni zawadi takatifu. Wakati roho zetu huko mbinguni zinapokuja katika dunia hii, “Zinaongezwa juu” (Abraham 3:26) ya mwili. Kama Nabii Joseph Smith alivyofundisha: “Tulikuja kwenye dunia hii ili tuweze kuwa na mwili na kuuwakilisha ukiwa msafi mbele ya Mungu katika Ufalme wa selestia. Kanuni kuu ya furaha inajumuisha kuwa na mwili. Ibilisi hana mwili, na hiyo ndiyo adhabu yake.”9

Kama Mzee David A. Bednar wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alivyo fundisha: “Miili yetu ya asili inawezesha kwa mapana, marefu, na wingi wa uzoefu ambao kiurahisi usingeweza kupatikana katika uwepo wetu kabla ya kuja hapa duniani. Hivyo, uhusiano wetu na watu wengine, uwezo wetu wa kugundua na kufanya kufuatana na ukweli, na uwezo wetu wa kutii kanuni na ibada za injili ya Yesu Kristo zinakuzwa kupitia maumbile ya kimwili. Katika shule ya mwili wenye kufa, tunapata uzoefu wa wema, upendo, upole, furaha, huzuni, masikitiko, maumivu, na hata changamoto za mapungufu ya kimwili katika njia ambazo zinatutayarisha kwa ajili ya maisha ya milele. Kiurahisi imesemwa, kuna masomo ambayo lazima tujifunze na uzoefu lazima tuwe nao, kama maandiko yanavyoeleza, ‘kulingana na mwili’ (1 Nefi 19:6; Alma 7:12–13).”10

Kwa nyongeza, kama Joseph Smith alivyofundisha, “Viumbe wote walio na mwili wana nguvu juu ya wale ambao hawana mwili.”11 Shetani anaweza kutujaribu, lakini hawezi kutulazimisha. “Ibilisi hana nguvu juu yetu mpaka pale tunapomruhusu.”12

Hatimaye, zawadi ya mwili uliokamilishwa, uliofufuliwa inasaidia kutuweka mbali na nguvu za shetani milele. Kama pasingekuwa na Ufufuko, roho zetu lazima zingekuwa chini ya utawala wa ibilisi, zisingeinuka kamwe. Na roho zetu lazima zingekuwa kama yeye, na tuwe maibilisi, malaika kwa ibilisi, kutengwa na uwepo wa Mungu wetu, na kuishi na baba wa uwongo, katika huzuni, kama yeye mwenyewe” 2 Nefi 9:8–9).

Roho na Mwili Sio Maadui

Ingawa zipo tofauti, roho na mwili hazistahili kuwa vitu viwili kimsingi tofauti na zenye uhalisia usioweza kupatanishwa. Kama Joseph Smith alivyo jifunza, “Hakuna kitu kama kitu kisicho na umuhimu. Roho yote ni maada, lakini ni safi mno au halisi na inaweza tuu kutambulika kwa macho safi zaidi, hatuwezi kuiona; lakini wakati miili yetu itakapo kuwa imetakaswa tutaona kwamba yote ni maada” (M&M 131:7–8).

Picha
Christ appears to the Nephites

Maelezo ya kina kutoka Christ Appearing in the West Hemisphere, na Armold Friberg

Katika hali Yake tukufu, na hali ya kufufuka, Yesu Kristo anawakilisha muungano mkamilifu wa roho na mwili akituonesha kwamba “Roho na mwili ni nafsi ya binadamu” (M&M 88:15). Katika maisha haya tunajitahidi kuwa “na mawazo ya kiroho” kuliko “mawazo ya kimwili” (2 Nefi 9:39), “[kuondoa] ubinadamu wa asili (Mosia 3:19), na “kuzuia tamaa [zetu] zote” (Alma 38:12). Lakini hiyo haimaanishi kwamba roho na mwili ni maadui. Kama Yesu Kristo alivyotuonesha, mwili sio wa kudharauliwa na kufanywa uvuke mpaka lakini utawaliwe na kubadilishwa.

Maisha katika Mwili wenye Kufa una Makusudi ya Maana

Fikra kwamba maisha haya ni majaribio zinaleta maana zaidi tunapo fikiria nini tunajua kuhusu maisha yetu kabla na baada ya hapa. Tuliishi kama roho kabla ya kuja duniani, na Baba wa Mbinguni ana kusudia tuwe kama Yeye na kuishi milele na maumbile ya kimwili yasiyo kufa. Kweli hizi zina maana kwamba muda wetu wa majaribio katika miili hii yenye kufa sio ya kiholela bali yana makusudi yenye maana ya kweli.

Kama Mzee Christofferson alivyoelezea: “Kwa chaguzi zetu tutaonesha kwa Mungu (na kwetu wenyewe) msimamo na uwezo wetu wa kuishi sheria yake ya kiselestia wakati tupo nje ya uwepo Wake na katika maumbile ya kimwili na nguvu zake zote, tamaa, na hamaki. Tungeweza kuuzuia mwili ili kwamba uwe kifaa kuliko kuwa mtawala wa roho? Tungeweza kuaminiwa kwa vyote katika muda huu na milele na nguvu za kimungu, ikijumuisha pamoja na uwezo wa kuumba uhai? Tungeweza sisi wenyewe mmoja mmoja kushinda uovu? Wale walioweza wangepata kuongezewa utukufu juu ya vichwa vyao kwa milele na milele’ [Ibrahimu 3:26]—kipengele chenye maana sana cha utukufu ule kuwa maumbile ya mwili uliofufuka, usio kufa, na mwili unaoshikika uliotukuka.”13

Uzoefu wetu katika miili yetu ya sasa, ukijumuisha mahusiano yetu sisi kwa sisi, yana maana kwa sababu yana fanana na yale ambayo yatakuja. Kama Joseph Smith alivyo jifunza, Kwamba uhusiano huu huu uliopo miongoni mwetu hapa utakuwepo miongoni mwetu kule, isipokuwa utazidishiwa utukufu wa milele, utukufu ambao sasa hatuufaidi (M&M 130:2).

Tunalo Tumaini katika Yesu Kristo

Picha
women at the tomb

The three Marys at the Tomb, na William-Adolphe Bouguereau, Superstock.com

Tangu pale kaburi tupu lilipoonekana, Ufufuko wa Yesu Kristo umeleta matumaini kwa sababu tunatambua katika Ufufuko Wake ni mategemeo yetu wenyewe ambapo yote [sisi] tuliyopoteza tutarejeshewa [sisi], ilimradi [sisi] tunaendelea kuwa waaminifu.14

Mitume wa awali wa Mwokozi waliweza kutoa ushahidi wa kijasiri wa Kufufuka Kwake kwa sababu waliuona na kuugusa mwili Wake. Lakini kulikuwa na mengi zaidi juu ya hilo kuliko hayo. Kama vile Yesu Kristo alivyokuwa ameponya udhaifu wa kimwili ili kuonesha kwamba alikuwa na uwezo wa kusamehe dhambi (ona Luka 5:23–25). Kufufuka Kwake—ushahidi wa kushikika wa uwezo Wake wa kushinda mauti ya kimwili—ukawa uhakikisho kwa wafuasi Wake juu ya nguvu Zake za kushinda mauti ya kiroho. Ahadi ambazo Yeye alizitoa katika mafundisho Yake—msamaha wa dhambi, amani katika maisha haya, uzima wa milele katika ufalme wa Baba—zikawa thabiti na imani yao haikuyumba.

“Kama Kristo hakufufuka, imani [yetu] ni bure” (1 Wakorintho 15:17). Lakini kwa sababu Yeye ali inuka kutoka kwa wafu, tunaweza “kuwa na tumaini kupitia upatanisho wa Kristo na uwezo wa kufufuka kwake, kuinuliwa kwenye uzima wa milele, na hii kwa sababu ya imani [yetu] kwake kulingana na ile ahadi (Moroni 7:41).

Wakati wa maisha Yake katika mwili wenye kufa, Yesu Kristo aliwaalika watu wamfuate Yeye. Baada ya Kifo Chake na Kufufuka, makusudio yakawa wazi zaidi. Kama sisi, kwa utiifu wa sheria na ibada za injili, tukakuza roho ya kiselestia ndani yetu, tunaweza kupokea mwili huo huo ambao ulikuwa mwili wa asili na {ukahuishwa kwa sehemu ya utukufu wa selestia [na] kisha kupokea huo huo hata utimilifu (M&M 88:28–29). Yeye ameonesha njia. Yeye ni njia. Ni kwa uwezo Wake—kupitia Upatanisho na Kufufuka- Kwake—kwamba ukamilifu huu wa selestia unawezekana, ambao unajumuisha ukamilifu wa furaha katika mwili uliofufuka.

Muhtasari

  1. Wakati Yesu Kristo alipowatokea watu katika Ulimwengu Mpya, Aliwaomba—maelefu yao—kumwendea, “mmoja mmoja,” na kugusa mikono Yake, miguu na ubavu wake ili kwamba waweze kushuhudia kwamba waliweza kugusa na kumwona Bwana mfufuka (ona 3 Nefi 11:14–15; 18:25).

  2. Teachings of Presidents of the Church: Joseph Smith (2007), 49.

  3. Ona Mwanzo 1:27; Kutoka 33:11; Matendo 7:56.

  4. Ingawa mawazo kama haya yalikuwepo katika imani za mwanzo za Kikristo, maelezo haya pekee yanakuja kutoka Makala thelathini na tisa za Kanisa la Angalikana (1563).

  5. Teachings: Joseph Smith, 42.

  6. JeffreyR. Holland, “The Only True God and Jesus Christ Whom He Hath Sent,” Liahona, Nov. 2007, 42.

  7. D. Todd Christofferson, “The Resurrection of Jesus Christ,” Liahona, Mei 2014, 113.

  8. Hata ufunuo wa Yesu Kristo kabla ya kuja duniani ulikuwa ni ushuhuda wa ukweli huu, kwa vile ulionesha kwamba mwili wa roho Yake ulikuwa wa kibinadamu kimaumbile (ona Etheri 3:16).

  9. Teachings: Joseph Smith, 211.

  10. David A. Bednar, “We Believe in Being Chaste,” Liahona, May 2013, 41.

  11. Teachings: Joseph Smith, 211.

  12. Teachings: Joseph Smith 214.

  13. D. Todd Christofferson, “Why Marriage, Why Family”, Liahona, Mei 2015, 51.

  14. Teachings: Joseph Smith, 51.

Chapisha