2017
Kumfikiria Yesu
April 2017


Kumfikiria Yesu

Mwandishi anaishi California, Marekani.

Picha
Thinking of Jesus

Mia alisisimka. Ilikuwa mara yake ya kwanza kanisani! Wamisionari waliieleza familia yake kuhusu Kanisa hili. Wao waliamua kuja.

Mia aliangalia huku na huko. Aliona nguo nyeupe juu ya meza. Kitu fulani kilikuwa chini yake.

“Nini kipo chini ya nguo ile?” Mia alimuuliza mmoja wa wamisionari.

Dada Hanson alitabasamu. “Ni sakramenti.”

Sakramenti. Hilo lilikuwa neno kubwa. Mia alikuwa amewasikia wamisionari wakiwaambia Mama na Baba yake kuhusu jambo hilo. Lakini hakuwa na uhakika ilikuwa na nini.

Kila mtu aliimba wimbo. Watu wawili waliifunua ile nguo nyeupe. Sinia la mkate lililikuwa chini yake! Mia aliwaona wakimega mkate vipande vipande.

Baada ya wimbo mtu mmoja mwanaume alisema maombi. Wanaume wengine walipitisha mkate kwa kila mtu.

“Mkate unatusaidia kukumbuka mwili wa Yesu,” Dada Garcia alinong’ona.

Mia alichukua kipande cha mkate. Alipiga picha akilini kuwa Yesu amesimama mbele yake.

Kisha kulikuwa na maombi mengine. Wanaume walipitisha sinia na vikombe vidogo vidogo vya maji.

“Maji yanatusaidia kukumbuka damu ya Yesu,” Dada Garcia alinong’ona. “Alikufa kwa ajili yetu kwa sababu Yeye anatupenda.”

Mia alichukua kikombe cha maji. Alifikiria ni kiasi gani Yesu alimpenda. Alihisi kama alikuwa anamkumbatia kwa nguvu.

Baadaye Dada Hanson alimpa Mia picha ndogo ya Yesu. “Tunakula mkate na kunywa maji kumkumbuka Yesu na kuahidi kumfuata. Alitabasamu. “Ulifikiria nini kuhusu Sakramenti?”

Mia aliitazama picha ya Yesu. Alikumbuka hisia nzuri alizozipata. Alitabasamu. “Zilikuwa nzuri! Ninampenda Yesu.”

Chapisha