2017
Jinsi ya Kupata Amani ya Kweli
April 2017


Majibu kutoka kwa Viongozi wa Kanisa

Jinsi ya Kupata Amani ya Kweli

Kutoka katika hotuba ya mkutano mkuu wa Aprili 2013.

Jesus Christ in a crowd

Matamanio ya kimbingu kwa watu wema kila mahali yamekuwa na siku zote yatazidi kuwa ni uwepo wa amani duniani. Kamwe tusikate tamaa katika kutimiza lengo hili. Lakini, Rais Joseph F. Smith (1838–1918) alifundisha, Kamwe haiwezekani kuwepo duniani Roho yule wa amani na upendo hadi wanadamu watakapo pokea ukweli wa Mungu na ujumbe wa Mungu, na kuutambua uwezo na mamlaka yake ambayo ni ya kimungu.

Kwa dhati tunatumaini na kuomba kwa ajili ya amani kote duniani, lakini ni kwa watu binafsi na familia ndiko tunakoweza kupata aina hii ya amani ambayo imeahidiwa kama zawadi ya haki. Amani hii ni zawadi iliyo ahidiwa kutokana na huduma na dhabihu ya Mwokozi ya kulipia dhambi.

Amani sio tu usalama au kukosekana kwa vita, ukatili, migogoro, na mabishano. Amani huja kutokana na kujua ya kwamba Mwokozi anajua sisi ni akina nani na anajua ya kwamba sisi tuna imani katika Yeye, tunampenda Yeye, na tunashika amri Zake, hata na hususani katikati ya majaribu na maafa makubwa (ona M&M 121:7–8).

Ninaweza kugeukia wapi ili nipate amani? Wapi kimbilio langu wakati vile vyanzo vingine vinakoma kunitibu? (“Where Can I Turn for Peace?” Wimbo, no. 129). Jibu ni Mwokozi, ambaye ni kiini na mwasisi wa amani. Yeye ni “Mfalme wa Amani” (Isaya 9:6).

Tukijinyenyekeza mbele ya Mungu, tukiomba daima, tukitubu dhambi zetu, tukiingia katika maji ya ubatizo na moyo uliopondeka na roho iliyovunjika, na kuwa wafuasi wa kweli wa Yesu Kristo ni mifano yenye maana sana ya haki ambayo huzawadiwa kwa amani ya kudumu.

Kanisa ni Mahali pa kukimbilia ambapo wafuasi wa Kristo hupata amani. Baadhi ya vijana duniani husema wao ni wa kiroho lakini sio wa kidini. Kujihisi kiroho ni hatua nzuri ya kwanza. Hata hivyo, ni Kanisani ambapo tunashirikishwa, tunafundishwa na kulishwa neno jema la Mungu. La muhimu zaidi, ni mamlaka ya ukuhani Kanisani ambayo inawezesha ibada na maagano matakatifu ambayo huunganisha familia pamoja na kufanya kila mmoja wetu afuzu kurudi kwake Mungu Baba na Yesu Kristo katika ufalme wa selestia. Ibada hizi huleta amani kwa sababu ni maagano na Bwana.

Mahekalu ni mahali ambapo nyingi kati ya ibada hizi hufanyika na pia ni kiini cha kimbilio la amani kutoka ulimwenguni. Wale ambao hutembelea viwanja vya hekalu au wanaoshiriki katika maonyesho ya nyumba za mahekalu pia huhisi amani hii.

Yesu Kristo ndiye kiini cha amani ya kweli. “Hata pamoja na majaribu ya maisha, kwa sababu ya Upatanisho wa Mwokozi na neema Yake, maisha ya haki yatazawadiwa kwa kuwa na amani binafsi (ona Yohana 14:26–27; 16:33).