2017
Je, Ni Jinsi Gani Naweza Kujifunza Akilini Mwangu na Moyoni Mwangu?
April 2017


Je, Ni Jinsi Gani Naweza Kujifunza Akilini Mwangu na Moyoni Mwangu?

Tafuta kujua ni nini unaweza kufanya wakati ukiwa na maswali.

girl with heart

Ni nini unapaswa kufanya wakati unapokuwa na swali kuhusu kitu fulani cha kimafundisho, kihistoria, au cha kibinafsi? Ni jinsi gani utapata jibu? Bwana anaahidi, “Mimi nitakujulisha wewe akilini mwako na katika moyo wako, kwa njia ya Roho Mtakatifu” (M&M 8:2). Ni kwa namna ganii waweza kutumia akili na moyo wako kutambua maongozi? Hapa kuna mawazo machache.

Akili

Jifunze, Omba, Sikiliza

Mzee Robert D. Hales wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alisema kwamba wakati tunapofanya uamuzi muhimu wa maisha Baba wa Mbinguni anatutegemea sisi kutumia haki yetu ya kujiamulia, tuichunguze hali ilivyo katika akili zetu kulingana na kanuni za injili, na kuleta uamuzi wetu Kwake katika maombi. (The Holy Ghost, Liahona, Mei 2016, 105).

Njia ni hyo hiyo kwa swali lo lote lile. Unaposoma, omba kwa moyo wa kweli kuhusu majibu utakayopata njiani. Roho Mtakatifu atakupa misukumo—ikiwa ni kwa fikra, au maneno akilini mwako au kumbusho nyingine za kibinafsi—ili kukuongoza hadi kwenye majibu zaidi unayohitaji.

Tumia Nyenzo

Chunguza maandiko, pamoja na Mwongozo wa Maandiko na misaada mingine ya kujifunza. Unaweza pia kuchunguza katika nyenzo nyingine za WSM kama vile hotuba za mkutano mkuu, Mada za Injili kwenye LDS.org, majarida ya Kanisa, Mradi wa Magazeti ya Joseph Smith, na zaidi. (Ona ukurasa 54 kwa orodha kutoka nyenzo za Kanisa.)

Zungumza

Usiwe na hofu katika kuomba msaada Mzee Ronald A. Rasband wa Akidi ya Mitume Kumi na Wawili alihamasisha, Mimi ninaenda kuwapeni changamoto. Unahitaji kufikiria juu ya mtu [ambaye anaweza kukusaidia kupata majibu]—rafiki unaye mwamini, mzazi au wazazi, babu na bibi, mwalimu, uaskofu, [au] mshauri … —na unahitaji maswali haya yajibiwe” (Face to Face broadcast, Jan. 20, 2016). Jaribu! Zungumza na mtu unaye mwamini kuhusu maswali yako na mtafute majibu kwa pamoja.

Moyo

Jifunze, Omba, Sikiliza

Hizi ndizo hatua muhimu za kutafakari akilini na moyoni mwako. Rais Dieter F. Uchtdorf, Mshauri wa Pili Katika Urais wa Kwanza, alisema, “Kama unataka kutambua ukweli wa kiroho, unatakiwa kutumia vifaa sahihi. Huwezi kupata uelewa wa ukweli wa kiroho na vifaa ambavyo havina uwezo wa kuugundua” (“Receiving a Testimony of Light and Truth,” Liahona, Nov. 2014, 22). Roho Mtakatifu ni kifaa ambacho kupitia kwacho tunajifunza mambo ya kiroho. Kwa hivyo unapo omba na kumsikiliza Roho, kwa wakati wake utaweza kupata majibu.

Kuwa Mvumilivu

Rais Uchtdorf pia alieleza, Kadiri tunavyozidi kuelekeza mioyo na mawazo yetu kuelekea kwa Mungu, ndivyo tunavyozidi kupewa mwanga mwingi wa mbinguni juu ya nafsi zetu. Pole pole kile mwanzo kilichoonekana kuwa na ukungu, giza, na kiko mbali kinakuwa wazi, chenye kung’aa na kilichozoeleka kwetu (Receiving a Testimony of Light and Truth, 22). Kutafuta majibu inaweza kuwa mchakato mrefu. Lakini ikiwa uko radhi kusikiliza ili kupata majibu, hata ikiwa itachukua muda, utapata.

Fanya Mazoezi ya Kutambua Misukumo

Unapozidi kutambua misukumo na kuwa tayari kuchukua hatua wakati Roho anapo kunong’oneza moyoni mwako, ndivyo inavyozidi kuwa rahisi kwako kutambua misukumo zaidi katika siku zijazo. Waweza “ukahisi kuwa hiyo ni sahihi” au ukahisi “mzubao wa mawazo” ikiwa siyo sahihi (ona M&M 9:8–9). Unaweza pia kuhisi kumbusho jepesi, hisia ya amani, au hisia nyingine ambayo ni maalum kwako. Bwana anakujua, na anajua jinsi utakavyo mwelewa Roho. Atakupa mwongozo wa kiupendo ambao ni wa kipekee kwako. Kwa hivyo endelea kusikiliza na kufanya mazoezi.