Skaidrite ni mmoja ya watu wenye furaha mno niliowahi kukutana nao. Maisha yake yanaonekana ni picha kamilifu. Lakini alipokuwa mtoto aliishi na mama yake mlevi, ambaye alikuwa hawezi kuwatunza yeye na dada yake. Skaidrite alishikilia mkono wa dada yake wakati dada akifa kutokana na njaa. Kuanzia umri wa miaka 8, Skaidrite aliishi katika nyumba mbali mbali za kulelea watoto. Alipigwa mateke, alipigwa bakora, na kuzuiwa kusali. Alitendewa kama mtumwa. Kwa miaka mingi, alifikiria sana kujiua.Miaka mingi baadaye, akitafuta matumaini, Skaidrite aliingia katika nyumba ya mikutano ya LDS.
Leslie Nilsson, mpiga picha
“Dada mmisionari aliniamkia na alitabasamu. Nilifikiri alikuwa ni malaika. Tangu siku ile maisha yangu yamebadilika. Hivi sasa imefikia miaka 17, na mawazo yote ya kumaliza maisha yangu yametoweka. Leo, mimi nina mawazo chanya. Ninapokuwa na masumbuko, ninayaweka kwa Mungu. Nimejifunza kumtegemea Yeye kwa kila kitu. Maisha ni mazuri kwangu.”
Picha
reflection in the mirror of looking out the window
Picha
standing in a kitchen with young boy
Picha
standing on the steps
Picha
walking down the hall
Picha
smiling at the camera
Ona picha kamili kwenye nyumba ya sanaa katika Maktaba ya mawasiliano
Ili kupata zaidi kuhusu kujizuiwa kujiua, tembelea Preventingsuicide.lds.org
Jifunze namna ya kuwatambua na kuwasaidia wale ambao yawezekana wanafikiria kujinyonga katika lds.org/go/41739.