2017
Kuwa Nuru
April 2017


Kuwa Nuru

“Inueni juu nuru yenu ili ing’are ulimwenguni. Tazama Mimi ni mwangaza ambao mtainua” (3 Nefi 18:24).

Picha
Be a light

Tunaweza kuwa nuru kwa wengine kwa kuwa rafiki wa kweli. Soma mawazo yaliyoko hapo chini na ongeza baadhi ya kwako mwenyewe. Kila wakati unapoandika jina la mtu fulani unaetaka kumwonyesha upendo, weka rangi zaidi kama ya jua.

  1. Wapende wengine: Unaweza kufanya mabadiliko makubwa katika maisha yao! Kristo ana wapenda wao, kwa hiyo jaribu kuwaonesha upendo huo.

    Nani: __________________________

  2. Samehe: Kama mtu fulani anakuumiza, jaribu kuona mambo kutoka kwenye mtazamo wao. Unaweza kuwasaidia wengine mioyo yao kulainika kama utasamehe.

    Nani: __________________________

  3. Watie moyo: Wasifie marafiki zako juu ya nguvu zao. Ona mazuri ndani yao hata kama wanahitaji kujiboresha. Kuwa kwako katika hali mzuri kunawasaidia pia!

    Nani: __________________________

  4. Msikilize Roho Mtakatifu: Maneno yako yanaweza kubadili hali mbaya kuwa mzuri. Roho Mtakatifu anaweza kukusaidia kujua nini cha kusema na jinsi ya kuonesha ukarimu.

    Nani: __________________________

  5. Kamwe usisengenye: Maneno mabaya yanaweza kuumiza. Wape wengine haki ya kutowatia hatiani kwa makosa, na puuza mawazo hasi.

    Nani: __________________________

  6. Wasaidie marafiki zako: Kuhudhuria tuu kwenye tukio la michezo ya rafiki zako au mchezo wa shule unaweza kuwasaidia kuhisi upendo wako.

    Nani: __________________________

  7. Waalike wengine kujifunza kuhusu injili: Hata kama hawakubali kile unachosema, wewe umeonesha kwamba unajali vya kutosha kushirikiana nao.

    Nani: __________________________

  8. Fanya urafiki na watu wa aina mbali mbali: Wengine wana mema mengi mno ya kushirikiana. Kristo alisaidia na kuwapenda watu wote bila kujali cho chote.

    Nani: __________________________

Chapisha