2017
Star Anang’ara
April 2017


Star Anang’ara

Mwandishi anaishi huko Colorado, Marekani.

“It’s nice to be here with you in Primary” (Kitabu cha Nyimbo za Watoto, 254).

Star Shines

Star alivuta nguo zake. Bado alijisikia vibaya kuvaa gauni kwenda kanisani. Katika kanisa lake la zamani, wasichana walivaa suruali au kaptula siku ya Jumapili. Lakini sio katika kanisa lake jipya. Yeye na mama yake walikuwa wamebatizwa tu katika Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho.

Star alivuta pumzi alipojitazama katika kioo. Alikuwa na msisimko wa kwenda kanisani mara ya kwanza kama muumini rasmi, lakini pia alikuwa na wasi wasi. Mwanzoni, alishinda na mamake muda wote kanisani. Lakini wakati huu alikuwa anaenda kwenye darasa la Watoto wa Msingi.

Star alipepesa macho kwa kivuli chake kwenye kioo. Itakuwaje kama hatapatana na wengine? Vipi kama watoto wengine hawangempenda?

“Star? Je uko tayari?” Mama alimwita.

Star alishuka ngazi “Je, naonekana vizuri?” aliuliza.

Mama alitabasamu. “Unaonekana mrembo.”

Star alifanya uso. “Unapaswa kusema hivyo. Wewe ni mama yangu.”

“Unasema kweli. Ninastahili kusema hivyo. Kwa sababu ni ukweli.”

Star alionyesha tabasamu dogo. Mama daima alikuwa na njia ya kumfanya ajihisi vyema. Lakini bado alikuwa anaogopa sana. Vipi kama hakukuwa na mtoto kati ya hao wengine aliyetaka kuzungumza naye? Alikuwa na marafiki shuleni lakini hawakuwa waumini wa kanisa lake jipya. Alitamani hata angalau angekuwa na rafiki hata mmoja wa kwenda pamoja naye kanisani.

“Nimekumbuka tu sasa hivi kitu fulani ninastahili kufanya,” alimweleza mama yake.

Alikimbia juu akipanda ngazi na kupiga magoti kando ya kitanda chake. “Baba wa Mbinguni mpendwa, tafadhali nisaidie nipate marafiki. Ninaamini yale wamisionari waliyonifundisha ni ya kweli, lakini mimi naogopa.”

Star alibaki amepiga magoti na kusikiliza. Baada ya muda alipata hisia tamu, yenye amani, na hakuwa na wasiwasi sana tena.

Kanisani Star na mama yake waliketi pamoja na familia iliyokuwa na wasichana watatu wadogo. Wazazi walijitambulisha na wakaanza kuzungumza na mama kabla ya mkutano kuanza. Star aliwasaidia wasichana wale kupaka rangi picha ya Yesu.

Askofu Andrews alielekea mahali walikokuwa. “Dada Cunningham! Star! Ni vyema kuwaona leo.” Aliwapa kila mmoja wao tabasamu zuri na kuwasalimia kwa mkono. Star alikuwa amesahau jinsi kila mtu kanisani alvyokuwa mzuri. Pengine atapata rafiki.

Baada ya mkutano wa sakramenti Star alienda kwenye darasa la Watoto wa Msingi. Aliwatazama wale watoto wengine akiwa na wasiwasi alipokuwa akiketi chini. Walikuwa wakizungumza wao kwa wao na walionekana kana kwamba hakuna aliyeonekana kumtambua. Moyo wa Star uliinama. Hata hivyo yeye atakuwa peke yake.

Mara msichana wa rika yake Star aliingia katika chumba hicho. “Anaonekana mwenye wasi wasi pia,” Star aliwaza. “Ninaweza kwenda kuzungumza naye.”

Star alivuta pumzi nzito, kisha akamkaribia yule msichana mgeni. “Mambo, jina langu ni Star. Mimi ni mgeni. Je ungependa kuketi na mimi?” Star aliishika pumzi yake. Je, msichana huyo angetaka kuwa rafiki yake?

Mdomo wa msichana huyo uliinuka kwa nusu tabasamu. “Mimi ni Sara. Mimi ni mgeni pia. Familia yangu imehamia tu hapa kutoka Ontario.”

“Mama yangu na mimi tulibatizwa wiki mbili zilizopita,” Star alisema. “Sina uhakika na ninacho hitajika kufanya.”

Tabasamu la Sara lilizidi kuwa kubwa. “Tutajua la kufanya pamoja.”

Star na Sara waliketi na wenzao darasani. Mara nyingine Star alimtazama machoni Sara na kutabasamu. Sara alitabasamu pia. Star alijisikia mtulivu na mwenye furaha. Alijua kwamba Baba wa Mbinguni alikuwa amejibu ombi lake na kumsaidia kupata rafiki.

Darasani mwalimu aliwataka Star na Sara wajitambulishe.

Star alisimama. “Jina langu ni Star Cunningham. Mama yangu nami tulibatizwa wiki mbili zilizopita.” Alipozi kidogo, na tabasamu likakua usoni mwake akimtazama rafiki yake mgeni. “Na huyu ni rafiki yangu Sara.”