Rafiki
Uchaguzi wa Jumapili
Julai 2024


“Uchaguzi wa Sabato,” Rafiki, Julai 2024, 4–5.

Uchaguzi wa Jumapili

“Sakramenti ni nini?” Anita aliuliza.

Hadithi hii ilitokea huko Isilandi

Picha
Wasichana wakiruka kwenye kifaa cha kuruka

“Juu zaidi!” Evolett alisema kwa rafiki yake Anita. Waliweza kuona ni juu kiasi gani waliweza kuruka kwenye kifaa cha Evolett

Hapo ndipo, Anita aliweza kuruka juu sana. Miguu yake ilipotua tena, ilifanya Evolett aruke juu! Wasichana wote wawili waligongana chini hatimaye. Wakacheka.

“Hii inafurahisha,” Anita alisema. “Je, tunaweza kucheza kesho pia?

Evolett akajiangusha mgongoni mwake. “Ndiyo! Ningependa tufanye hivyo.”

“Tunaweza kucheza nyumbani kwa bibi yangu.” Bibi yake Anita aliishi nyumba kadhaa kutoka kwa Evolett.

Kisha Evolett akakumbuka kuwa siku inayofuata ilikuwa Jumapili. Alitaka kwenda kwenye darasa la Watoto. Ingekuwa burudani kucheza na Anita, lakini yeye alitaka kufanya chaguzi nzuri.

“Nimekumbuka kwamba sitaweza,” Evolett alisema. “Samahani. Ninakwenda kanisani pamoja na familia yangu kesho.”

Anita alisimama na kujiangusha tena. “Kwa nini?”

Evolett akaanza kuruka pia. “Ndiyo, ninataka kumfuata Yesu Kristo. Familia yangu inaenda kanisani kila Jumapili ili kujifunza kuhusu Yeye na kupokea sakramenti.”

“Sakramenti ni nini?” Anita aliuliza.

“Huo ni wakati tunapokula kipande kidogo cha mkate na kunywa kikombe kidogo cha maji ili kumkumbuka Yesu Kristo,” alisema Evolett. “Kisha watu wanazungumza kuhusu namna gani Yesu anawasaidia. Na baada ya hapo, kuna darasa maalumu kwa ajili ya watoto!”

“Hiyo inaonekana kuwa ya kufurahisha!” Anita alisema. “Je, ninaweza kuja?”

“Hakika!” Evolett alitabasamu.

Anita alikimbia nyumbani kumwuliza bibi yake kama angeweza kwenda Jumapili pamoja na Evolett. Asubuhi iliyofuata, Evolett na familia yake walimchukua Anita njiani.

Walipofika kanisani, Evolett alimtembeza Anita kuzunguka maeneo ya kanisa. Alimwonyesha chumba cha darasa la Watoto, chumba cha mazoezi na chumba cha ibada.

Punde ulifika muda kwa ajili ya mkutano wa sakramenti. Evolett na Anita walikaa pamoja. Evolett alijaribu kufikiria juu ya Yesu Kristo wakati wa sakramenti. Kisha walisikiliza mahubiri.

Picha
Mzungumzaji wa mkutano wa sakramenti na wasichana wakikutana na mwalimu wa Darasa la Watoto

Mwishowe ukafika muda kwa ajili ya darasa la Watoto! Evolett alimtambulisha Anita kwa baadhi ya marafiki zake.

“Huyu ni rafiki yangu Anita,” Evolett alisema.

“Tumefurahi sana umekuja leo. Mimi ni Dada Magnusson,” mwalimu wa darasa la Watoto alisema.

Evolett na Anita walipokuwa wakisikiliza somo kuhusu Yesu Kristo, Evolett alihisi furaha ndani yake. Alipenda kuwa kanisani pamoja na Anita. Aligeuka na kutabasamu kwa Anita. Naye alirudisha tabasamu.

“Asante kwa kunikaribisha,” Anita alisema wakiwa njiani kurudi nyumbani.

Evolett alifurahi kwa kuweza kumfuata Yesu Kristo. Na alifurahi kwamba Anita alitaka kujifunza kumhusu Yeye pia.

Ilikuwa burudani kuruka juu ya kifaa cha kuruka na kuelea angani, lakini hisia nzuri Evolett alizohisi ndani yake zilikuwa bora zaidi.

Picha
Trei ya sakramenti na msichana anayeangalia juu na kuonekana mwenye amani
Picha
PDF ya hadithi

Vielelezo na Fiona Powers

Chapisha