Rafiki
Sauti Kubwa na Rangi Angavu
Julai 2024


“Sauti Kubwa na Rangi Angavu,” Rafiki, Julai 2024, 10–11.

Sauti Kubwa na Rangi Angavu

“Kwa nini Baba wa Mbinguni hafanyi makelele makubwa yatoweke?” Charlotte aliuliza.

Hadithi hii ilitokea huko Marekani.

Charlotte alichukia makelele! Hakupenda jinsi sauti zilivyopiga kwa nguvu katika masikio yake au mwangwi kichwani. Hata alipojua kwamba yuko salama, bado alihisi woga pale magari yalipotoa sauti kali wakati yakifunga breki kwa ghafla na kwa nguvu.

Na Charlotte hakika hakupenda fataki!

Familia yake ilijaribu vitu vingi sana ili kumpa faraja wakati palipokuwa na makelele. Baba alimnunulia kiziba masikio maalumu ili kusaidia kuzuia kelele. Kukiwa na radi, Mama alimkumbatia na kujificha pamoja naye. Charlotte pia alisali kwa ajili ya kuomba usaidizi ili asiogope.

Vitu hivi vyote vilisaidia. Lakini sauti kali bado zilimfanya ahisi kuogopa.

“Tunakwenda kwenye maonyesho maalumu ya fataki kwenye uwanja wa bustani usiku wa leo,” Mama alimwambia Charlote. “Je, unataka kuja?”

Charlote alikunja uso. “Lakini fataki zina sauti kali.”

“Sasa kwa vile wewe ni mkubwa, fataki inaweza kuwa burudani kuangalia,” Mama alisema. “Marafiki zako wote watakuwa pale. Tunaweza kuleta vifaa vyako maalumu vya kuziba masikio. Je, unadhani utaweza kujaribu?”

Charlotte alishusha pumzi. “SAWA. Nadhani ninaweza kujaribu.”

Maonyesho ya fataki kwenye uwanja wa bustani yalianza vizuri. Charlotte na marafiki zake walikimbia kimbia uwanjani kwenye nyasi, wakishirikiana vitafunwa na kucheza michezo. Punde anga likawa giza. Charlotte alikaa chini na kuvuta vifaa vyake maalumu vya kuziba masikio akiangalia kwa woga angani.

BOOM! BOOM! PASUKA!

Charlotte moyo wake ulipiga kwa haraka zaidi, na alihisi kifua chake kubana. Aliruka juu na alijaribu kukimbia mbali na yale mabomu yaliyomzunguka.

Mama alimkimbilia Charlote na kumkamata. Walirudi na kukaa chini, na Mama akamkumbatia kwa karibu. Machozi yalianguka usoni mwa Charlotte.

“Nasikitika hilo limekuogopesha wewe,” Mama alisema. “Niko hapa tu. Acha tufokasi juu ya rangi ili usisikie sauti zaidi. Unaona nini kwa macho yako?

Charlotte alivuta pumzi kubwa. “Naona dhahabu, na nyekundu, na kijani.”

“Sasa tumia pua yako,” Mama alisema. “Unavuta harufu gani?”

“Ninaweza kusikia harufu ya moshi na nyasi,” alisema Charlotte. “Na bisi!”

“Ni hisia gani nyingine unaweza kutumia sasa hivi?”

Charlotte alifumba macho yake. “Ninaweza kuhisi. Fataki zinapolipuka, ninaweza kuhisi kifua changu kinatikisika.”

“Je, unaweza kuonja kitu chochote?” Mama aliuliza.

Charlotte alitoa ulimi wake nje. “Siwezi kuonja hizi fataki.” Alicheka.

Vyote hivi vilimfanya Charlotte kuwa na hamu ya kujua. Watu wanazifanyeje hizi rangi tofauti? Alijiuliza kwa mshangao. Kwa nini fataki zinalipuka? Je, ni kwa jinsi gani zinatengeneza maumbo tofauti? Fataki hazikuonekana kutisha tena sasa.

“Mama, fataki ni za kushangaza!” Charlote alisema.

Picha
Msichana mwenye vifaa vya kuziba masikio na mama wamelala kwenye kilima chenye nyasi wakitazama fataki kwa pamoja.

Mama alipokuwa akimlaza Charlote kitandani usiku ule, Charlotte aliuliza, “Kwa nini Baba wa Mbinguni hajajibu sala zangu nilipomwomba kuyaondolea mbali makelele?”

Mama aliwaza kwa muda. “Baba wa Mbinguni siyo daima atayaondoa mbali mambo yanayotisha,” alisema. Lakini wakati mwingine Yeye anatusaidia sisi kuona mambo katika njia tofauti au kutupatia watu wanaosaidia kutufariji.”

“Kama vile alivyonisaidia mimi usiku wa leo!” alisema Charlotte

“Hiyo ni sawa!” Mama alitabasamu. “Ulienda kwenye onyesho la fataki licha ya kuwa unaogopa. Ndipo Baba wa Mbinguni amekusaidia kutuliza hofu yako. Yeye pia amekusaidia kuona uzuri wa fataki kwa kutumia milango yako mingine ya fahamu.

Charlotte alifikiria juu ya rangi angavu katika anga na kutabasamu. Bado hakutaka sauti kubwa. Bado zilimwogopesha Lakini alijua Baba wa Mbinguni daima angeweza kumsaidia kuwa jasiri.

Picha
PDF ya hadithi

Kielelezo na Adam Howling

Chapisha