Rafiki
Shughuli za Jumapili
Julai 2024


“Shughuli za Jumapili,” Rafiki, Julai 2024, 17.

Kitu cha kuburudisha

Shughuli za Jumapili

Picha
Ubao wa Shughuli na vielelezo

Vielelezo na Josh Talbot

Rusha kitu kidogo, kama vile punje ya harage au sarafu, juu ya ukurasa. Kisha fanya shughuli ambayo kitu hicho kitatua juu yake. Ukimaliza, jaribu tena! Endelea hadi upate mara nne mfululizo.

  • Soma hadithi kutoka katika jarida la Rafiki.

  • Nendeni matembezi kuona mazingira asili pamoja na familia yako.

  • Tazama picha za mahekalu.

  • Cheza mchezo na familia yako.

  • Jifunze wimbo mpya wa Watoto.

  • Andika barua kwa mmisionari.

  • Orodhesha vitu 10 ulivyo na shukrani juu yake.

  • Chora picha ya familia yako.

  • Mwombe mzazi wako akusimulie hadithi ya familia.

  • Mpigie simu mwanafamilia anayeishi mbali.

  • Soma maandiko nje ya nyumba.

  • Andika ujumbe wa shukrani kwa mtu.

  • Jenga hekalu kwa kutumia vibao au vijiti.

  • Igiza hadithi ya maandiko.

  • Mtembelee mtu aliye mpweke au mwenye shida.

  • Tengeneza vitafunwa na uwapelekee majirani zako.

  • Angalia video ya maandiko kwenye ChurchofJesusChrist.org.

  • Imbeni wimbo wa Watoto au nyimbo za dini.

  • Fanya jambo zuri kwa ajili ya mtu katika familia yako.

  • Fanya shughuli iliyoko katika ukurasa wa shughuli wa jarida la Rafiki.

  • Andika ushuhuda wako.

  • Saidia familia yako kuandaa chakula au asusa.

  • Paka rangi picha au andika ujumbe wa shukrani kwa mwalimu wa Darasa la Watoto.

  • Kariri Makala za Imani

  • Tengeneza kolagi ya picha kutoka kwenye jarida la Rafiki.

Chapisha