Rafiki
Abishi Alikuwa Nani?
Julai 2024


“Abishi Alikuwa Nani?” Rafiki, Julai 2024, 24–25.

Jifunze kuhusu Kitabu cha Mormoni

Abishi Alikuwa Nani?

Picha
Abishi ameshikilia chungu

Abishi alikuwa Mlamani. Alifanya kazi kwa malkia na mfalme.

Picha
Abishi akimwangalia Amoni anafundisha

Siku moja Abishi alimwona Amoni akiwafundisha kuhusu Yesu Kristo. Wote waliomsikiliza walihisi Roho kwa nguvu sana hata kwamba walianguka ardhini.

Picha
Abishi akiangalia kwa mshangao watu walioanguka ardhini

Abishi tayari aliamini katika Yesu Kristo. Alijua kwamba nguvu za Mungu ziliwafanya wengine kuanguka ardhini.

Picha
Abishi akizungumza na watu nje

Alikimbia nje na kuwaambia watu njooni muone muujiza ambao umetokea kwa malkia na mfalme.

Picha
Abishi akimsaidia malkia kusimama wima

Alimsaidia malkia kusimama.

Picha
Mfalme na malkia wakizungumza na watu

Mfalme na malkia walitoa shuhuda zao juu ya Yesu Kristo kwa wengine. (ona Alma 19:16–17, 28–31.)

Changamoto ya Maandiko

  • Je, ni nani alimfundisha Mfalme Lamoni kuhusu Mungu? (Alma 18:26–28)

  • Je, ni jina gani jipya Walamani walijiita wenyewe baada ya kumfuata Yesu Kristo? (Alma 23:17)

  • Je, watu walizika kitu gani katika Alma 24:19?

Ninaweza Kusoma Kitabu cha Mormoni!

Picha
Ukurasa wa kupaka rangi wa watu wakizika silaha zao.

Baada ya kusoma, paka rangi sehemu ya picha. Unaweza kusoma maandiko haya yanayoenda sambamba na usomaji wa kila wiki kutoka Njoo, Unifuate.

Picha
PDF ya hadithi

Vielelezo na Bryan Beach

Chapisha