Rafiki
Mimi Ninapendwa
Julai 2024


“Mimi Ninapendwa,” Rafiki, Julai 2024, 42.

Imeandikwa na Wewe

Mimi Ninapendwa

Picha
Msichana mwenye tabasamu akiwa na begi mgongoni mbele ya shule

Nimekuwa na matatizo ya kiafya ambayo yamekuwa magumu sana. Nilizaliwa tofauti, pasipo viungo vya haja. Nimekuwa na upasuaji mkubwa mara tatu, na ndogo kadhaa.

Wakati mwingine ninajiuliza kwa nini mimi niko hivi, lakini nikifikiria kuhusu Mungu na mpango Wake wa wokovu inanisaidia kukumbuka kwamba mimi ninapendwa kama mtu mwingine yeyote. Kuwa na ushuhuda juu ya injili ni vizuri sana, na ninajua ninaweza kumtegemea Bwana.

Ninaupenda sana mwili wangu. Ninajua hakika mimi ni zawadi ya nuru (ambayo ndio maana ya jina langu) Japokuwa ninapambana, ninajua ninaweza daima kumwomba Mungu kwa ajili ya msaada.

Picha
PDF ya hadithi

Kielelezo na Alyssa Johnson

Chapisha