Rafiki
Shughuli za Njoo, Unifuate
Julai 2024


“Shughuli zaNjoo, Unifuate ,” Rafiki, Julai 2024, 28–29.

Shughuli za Njoo, Unifuate

Kwa ajili ya jioni ya nyumba, ni au kujifunza maandiko—au kwa ajili ya burudani tu!

Julai 1–7

Sanaa ya Mpango wa Furaha

Kwa ajili ya Alma 17–22

Picha
Mikono ya mtoto kwa maumbo ya karatasi yaliyokatwa

Haruni na Amoni wote wawili walifundisha kuhusu mpango wa furaha wa Baba wa Mbinguni. Wao waliuita mpango wa ukombazi (ona Alma 18:36–39 na Alma 22). Geuza ukurasa wa 12 ili kutengeneza sanaa yako ya mpango wa furaha.

Julai 8–14

Vyombo Mikononi mwa Mungu

Kwa ajili ya Alma 23–29

Picha
Watoto wakitengeneza vyombo vinavyotengenezwa nyumbani

Amoni alisema kwa kaka zake, “Sisi tumefanywa vyombo katika mikono ya Mungu kutimiza kazi hii kubwa” (Alma 26:3). Kusanya vitu unavyoweza kuvitumia kutengeneza muziki. Kisha ufanye midundo na nyimbo. Kama vile tu tunavyotumia vyombo kufanya muziki, Mungu anaweza kututumia sisi kusaidia kujenga Kanisa la Yesu Kristo.

Julai 15–21

Kumbusho la Viti vya Muziki

Kwa ajili ya Alma 30–31

Picha
Watoto wanatembea kuzunguka viti

Alma alifundisha kwamba “vitu vyote vinaonyesha kwamba kuna Mungu” (Alma 30:44). Hiyo inamaanisha kwamba kila kitu Mungu alichokiumba kinatukumbusha juu Yake. Panga viti katika duara kukiwa na viti vya kutosha kwa kila mtu isipokuwa mtu mmoja. Mtu mwingine na apige muziki na kuchagua wakati gani azime. Muziki unapozima, kila mtu anakaa kwenye kiti. Mtu ambaye anakosa kiti anashiriki kitu kimoja ambacho kinawakumbusha juu ya Mungu. Endelea hivyo mpaka kila mmoja amepata zamu ya kushiriki.

Julai 22–28

Kukuza Ushuhuda Wako

Kwa ajili ya Alma 32–35

Picha
Mtoto anachora picha

Alma alifundisha kwamba unaposikiliza neno la Mungu na kufanya vitu ili kuonyesha imani yako, ushuhuda wako utakua, kama mti (ona Alma 32:37). Chora vitu unavyoweza kufanya ili kusaidia mti kukua, kama kuupatia maji, na mwangaza wa jua. Kisha chora vitu unavyoweza kufanya ili kusaidia ushuhuda wako kukua, kama kwenda kanisani na kusali.

Picha
PDF ya hadithi

Vielelezo na Katy Dockrill

Chapisha