Rafiki
Kushiriki Kitu Unachoamini
Julai 2024


“Kushiriki Kitu Unachoamini,” Rafiki, Julai 2024, 2–3.

Kutoka Urais wa Kwanza

Kushiriki Kitu Unacho Amini

Imechukuliwa kutoka “A Child and a Disciple,” Liahona, Mei 2003, 29–32.

Mwanaume ubaoni

Baba yangu alikuwa mwanasayansi. Wakati mmoja nilisoma hotuba ambayo aliitoa kwa kikundi kikubwa cha watu. Ndani yake, aliongelea juu ya Uumbaji na Muumba kama alivyozungumza kuhusu sayansi. Nilijua kuwa wachache katika kikundi kile walishiriki imani yake. Hivyo kwa mshangao nilimwambia, “Baba, ulitoa ushuhuda wako.”

Aliniangalia, akiwa na mshangao usoni pake na kusema, “Nimefanya hivyo?” Hakuwa hata amejua kuwa amekuwa jasiri. Alikuwa amesema kitu alichojua kuwa ni cha kweli.

Sisi sote ambao tumebatizwa tumeahidi kushiriki injili. Tunaweza kusali kwa imani ili tuweze kuhisi upendo wa Mwokozi kwa ajili yetu na kwa ajili ya wote tunaokutana nao. Utafurahia kuhusu Kanisa la Bwana na kazi Yake, na itajionyesha. Kusema kile unachoamini itakuwa ni sehemu ya wewe ulivyo.

Njia Rahisi za Kushiriki

Unaweza kushiriki injili katika njia nyingi. Andika kitu ambacho ungesema kwa kila mtu ili kushiriki kitu anachoamini. Kitu cha kwanza kimefanywa kwa ajili yako.

Wikiendi yako ilikuwaje?

Vizuri! Nilienda kanisani.

Watu wengi wana imani tofauti za kidini. Je, wewe unaamini nini?

Papi wangu ni mgonjwa. Je, wewe utasali kwa ajili yake?

Shughuli ya PDF inawaonyesha wasichana wawili wakiongea, msichana amenyanyua kidole shuleni, na wavulana wawili wakiwa wanaongea

Vielelezo na Alyssa Tallent