Rafiki
Sanaa ya Mpango wa Furaha
Julai 2024


“Sanaa ya Mpango wa Furaha,” Rafiki, Julai 2024, 12–13.

Kitu cha kuburudisha

Sanaa ya Mpango wa Furaha

Picha
PDF ya hadithi

Vielelezo na Marina Pessarrodona

Fanya sanaa hii ili ikusaidie kufundisha mpango wa furaha wa Baba wa Mbinguni. Unaweza kusoma kuhusu mpango huu katika Alma 18:36, 39 na Alma 22:8–16.

  1. Kata vipande hapo chini kwenye mistari ya nukta. Toboa tundu kwenye kila duara nyeupe.

  2. Funga kamba kupitia tundu ili kuunganisha vipande pamoja na maneno na picha inayoendana nayo. Funga kamba nyingine kupitia tundu la juu.

  3. Funga kamba hizo zote kwenye kijiti. Kisha ning’iniza sanaa yako.

Uumbaji. Mungu aliumba mbingu na nchi na vitu vyote vilivyomo.

Anguko. Adamu na Hawa walichagua kula kutoka kwenye mti wa ujuzi wa mema na mabaya. Hii iliwapa wao kuwa na familia.

Maisha Duniani. Sote tulizaliwa duniani ili kujifunza na kukua.

Upatanisho wa Yesu Kristo. Yesu Kristo alikuja duniani. Kama sehemu ya Upatanisho Wake, Yeye aliusikia uchungu wetu wote na alilipia dhambi zetu. Alikufa na anaishi tena. Kwa sababu yake Yeye, sisi tunaweza kutubu na kuishi na Baba wa Mbinguni baada ya kufa.

Chapisha