“Kumfuata Yesu kwa Pamoja,” Rafiki, Julai 2024, 20–21.
Kumfuata Yesu kwa Pamoja
Watoto huko Pedro Domingo Murillo Province, Bolivia, walijifunza kuhusu umuhimu wa kujiandaa kwa ajili ya hekalu. Walitengeneza michoro na maumbo ya kile walichofikiria siku za baadae za Hekalu La Paz Bolivia litakavyoonekana.
Lily M., umri miaka 10, Arizona, Marekani
“Moroni Anazika Mabamba ya Dhahabu,” Arthur S., umri miaka 6, Alaska, Marekani
“Nyumba ya Bwana,” Audrey B., umri miaka 9, Alberta, Kanada
“Silaha za Mungu,” Ethan M., umri miaka 10, Virginia, Marekani
“Ubatizo,” Quinn S., umri miaka 8, Colorado, Marekani
“Bustani ya Edeni,” Abigail B., umri miaka 10, Kansas, Marekani
Nilimhisi Roho Mtakatifu wakati ninaposikiliza mahubiri kanisani.
Serfina K., umri miaka 9, Mkoa wa Mwanza, Tanzania
Mababu zangu walisafiri hadi Utah pamoja na msafara wa mikokoteni. Nimetengeneza mkokoteni ili kukumbuka mambo mazuri waliyoyafanya.
Maddie J., umri miaka 9, Utah, Marekani
Tunavyo vitabu vingi nyumbani, lakini kitabu tunachokisoma mara nyingi zaidi ni Kitabu cha Mormoni. Nilijifunza kutoka kwa baba yangu kwamba kila wakati unaposoma Kitabu cha Mormoni utajifunza mambo mapya.
Louie C., umri miaka 10, Wilaya ya Taoyuan, Taiwani
Sikuweza kuviona viatu vyangu na nilisema sala nipate usaidizi. Nilifikiri jibu lingekuja mara moja, lakini halikuja. Nilichanganyikiwa, hivyo nilichukua shati lililokuwa sakafuni na kulitupa. Chini ya shati langu vilikuwepo viatu vyangu! Sala zangu hazikujibiwa kwa njia niliyotegemea, lakini nilijua sala yangu imesikiwa.
Cosette K., umri miakka 10, Queensland, Australia
Nilipanda maua kwa ajili ya dada katika ujirani wetu na kulisha paka wake. Nilihisi furaha ya kuhudumu kama Yesu alivyofanya.
Matías V., umri miaka 8, Santiag Metropolitan Region, Chile