Rafiki
Raina Anajaribu Tena
Julai 2024


“Raina Anajaribu Tena,” Rafiki, Julai 2024, 36–37.

Raina Anajaribu Tena

“Hiyo itakuwa mara ya mwisho kujaribu kitu chochote kipya tena,” Raina alisema.

Hadithi hii ilitokea huko Marekani.

Raina alisoma maneno yaliyo kwenye kipeperushi shuleni kwao tena. Shindano la Insha: Shinda safari ya bure kwenda Jijini New York!

Lilikuwa shindano kwa ajili ya wanafunzi wa shule nyingi katika eneo lile. Raina akajifikiria yeye mwenyewe katika Jiji la New York, akiwa amezungukwa na maghorofa marefu na sanamu ya Uhuru karibu yake. Alitaka kwenda!

“Lazima uingie,” Sydney alisema. “Wewe ni mwandishi bora zaidi katika darasa letu”

Maneno ya Sydney yalimfanya ahisi vizuri. Raina hakujua mengi kuhusu kuandika insha. Lakini alitaka kujaribu.

Baada ya shule, Raina alikaa kwenye dawati lake. Gonga, gonga, gonga. Aligonga gonga penseli yake juu ya karatasi alipokuwa akitafakari kuhusu mawazo yake. Mwishowe, akaanza kuandika.

Ilimchukua wiki nzima kwa Raina kumaliza. Lakini kwa msada kutoka kwa mama, mwishowe alihisi yuko tayari kuwasilisha insha yake.

Wiki kadhaa zilipita. Raina alikuwa na shauku ya kuona nani ameshinda. Labda hivi karibuni atakuwa anaelekea New York.

“Wanafunzi zaidi ya mia moja waliingia,” Bwana Wright alisema kutokea mbele ya darasa. “Asante kwenu nyote ambao mliandika insha.”

Moyo wa Raina ulidunda kwa shauku.

“Ingawa hakuna mwanafunzi wetu yeyote aliyeshinda shindano hili, Raina amekuwa katika tano bora ya washindani wote. Hongera, Raina,” Bwana Wright alisema.

Raina alitabasamu wakati wanafunzi wenzake darasani wakipiga makofi. Lakini ndani alikuwa amekunja uso. Kuwa katika tano bora haikuwa vizuri kama kushinda. Ndoto yake ya kuiona New York ilitoweka.

Raina alipofika nyumbani, alijibwaga kwenye kiti jikoni karibu na wazazi wake. “Nimepoteza shindano lile,” yeye alisema. “Hiyo ni mara mwisho katu sitajaribu tena kitu chochote kipya tena. Nitafanya kile tu ninachojua nakiweza vizuri.” Akafunika kichwa chake kwa mikono yake.

Picha
Msichana mwenye huzuni kwenye meza ya jikoni pamoja na wazazi

“Nasikitika hukuweza kushinda,” Mama alisema. Mama na mimi sote wawili tunajivunia wewe kwa kujaribu,” Baba alisema. Baba alikaa chini pembeni ya Raina. “Unakumbuka wakati nilipokuwa sina kazi miaka miwili hivi iliyopita?”

Raina aliitikia kwa kichwa.

“Nilituma maombi ya kazi sehemu nyingi, na sikupata ajira kwa zote nilizoomba,” Baba alisema. “Nilihisi kukata tamaa sana.”

Raina aliinua kichwa chake. “Kweli?”

Baba aliitikia kwa kichwa. “Lakini sikukata tamaa. Baada ya muda mrefu, nilipata kazi ambayo ilikuwa bora. Lakini isingetokea kama ningeacha kujaribu.”

Mama akaweka mkono wa faraja mgongoni pa Raina. “Je, unajua ni hadithi ngapi ninazituma kwenye magazeti tofauti tofauti?” aliuliza. “Na ni ngapi zinakataliwa? Lakini siwezi kukata tamaa kama ninataka kuona kazi yangu inachapishwa. Kuandika ni muhimu kwangu mimi, hivyo naendelea kujaribu.”

Raina daima amekuwa akifikiri wazazi wake ni wazuri katika kila kitu walichokifanya. Hakuwa amejua kwamba wamewahi kukataliwa pia.

Bado alikuwa na huzuni, lakini ilionekana si vyema kuacha kujaribu tena. Hicho hakikuwa kitu ambacho Baba wa Mbinguni alikitaka kwake. Raina aliamua asingeweza kukata tamaa. Angeweza kujaribu vitu vingine zaidi, hata vitu ambavyo hakufanya vyema mara moja.

“Nafikiri nitaingia kwenye shindano tena mwaka ujao,” Raina alisema. Kupoteza shindano hakupaswi kuwa mwisho wa ndoto zake.

Raina alienda mezani pake na akachukua penseli yake. Kuandika kumekuwa jambo la burudani. Gonga, gonga, gonga. Ni jambo gani jipya analoweza kuandika tena?

Picha
Msichana mwenye tabasamu amekaa mezani akiwa na penseli na karatasi.
Picha
PDF ya hadithi

Vielelezo na Vivian Mineker

Chapisha