Rafiki
Salamu kutoka Nikaragua
Julai 2024


“Salamu kutoka Nikaragua!” Rafiki, Julai 2024, 8–9.

Salamu kutoka Nikaragua!

Jifunze kuhusu watoto wa Baba wa Mbinguni ulimwenguni kote.

Nikaragua ni nchi iliyoko Amerika ya Kati. Takribani watu milioni 7 wanaishi huko!

Lugha

Jalada la Kihispania la jarida la Rafiki

Lugha rasmi ni Kihispania Baadhi ya watu pia huongea lugha za asili kama vile Kimiskito, Kisumo na Kirama.

Kueneza Injili

Picha ya eneo la ujenzi wa hekalu na kielelezo cha watoto wakisoma pamoja

Wamisionari wa kwanza walikwenda Nikaragua mwaka 1953. Sasa kuna zaidi ya waumini 100,000 huko! Huko kuna hata hekalu lililo katika hatua za ujenzi.

Papa wa Ziwa Nikaragua

Picha za Ziwa Nikaragua na kielelezo cha papa

Papa aina ya Bull wanaweza kuishi katika maji ya bahari na maji baridi. Hii inamaanisha wanaweza kuishi katika bahari, mito na maziwa. Wao wanaogelea kutoka Bahari ya Atlantiki kupitia mto mrefu na kuishi katika Ziwa la Nikaragua.

Palo de Mayo

Picha ya nguzo iliyorembeshwa kwa riboni za rangi na kielelezo cha wingu la mvua.

Watu huko Nikaragua wanafanya sherehe kubwa ziitwazo Palo de Mayo majira ya mvua yanapokuja. Wanaupamba mti au nguzo kwa riboni za rangi nyingi na kucheza kuuzunguka na kuwa na burudani ya mwezi mzima.

PDF ya hadithi

Vielelezo na Dave Klüg