Rafiki
Mazungumzo na Alan kuhusu Makala ya Imani
Julai 2024


“Mazungumzo na Alan kuhsu Makala ya Imani,” Rafiki, Julai 2024, 40–41.

Mazungumzo na Alan kuhusu Makala ya Imani

Alan anatoka Málaga, Hispania. Tulimuuliza maswali kadhaa kuhusu jinsi alivyojifunza Makala ya Imani.

Picha
Picha ya Alan

Tuambie kuhusu wewe mwenyewe.

Picha
Mvulana aliyevalia koti la maabara akiwa na bika.
Picha
Sahani ya omeleti ya Kihispania

Nina umri wa miaka minane. Nitakapokuwa nimekua, nataka kuwa mwana sayansi maarufu. Rangi niipendayo ni rangi ya chungwa, na chakula nikipendeleacho ni tortillas de patatas (omeleti ya Kihispania) upishi wa bibi yangu.

Je, ulijifunzaje Makala ya Imani?

Nilianza kujifunza katika darasa la Watoto. Tuliimba nyimbo ili kutusaidia kuzikariri. Nyakati zingine walimu wetu waliziandika ubaoni na kufuta baadhi ya maneno. Pia tulichora picha ili kuelezea kile ambacho kila Makala ya Imani ilimaanisha.

Pia tulifanyia mazoezi kuzisema pamoja na familia yangu ndani ya gari tukiwa njiani kwenda shule. Ninamsaidia dada yangu mdogo, Maia, kujifunza hizo pia. Naye pia anazijua sita za mwanzo!

Ni Makala ya imani ipi uipendayo?

Picha
Mvulana akiwa ameketi kwenye meza na kitabu kikiwa kimefunguliwa

Ninaipenda namba tisa. Tunaamini yale yote Mungu aliyoyafunua, na ambayo sasa anayafunua, na tunaamini kwamba bado Yeye atayafunua mambo mengi makuu na muhimu yahusuyo Ufalme wa Mungu. Inafundisha kwamba Baba wa Mbinguni anayo mambo mengi kwa ajili yetu kujifunza kidogo kidogo.

Ni kwa jinsi gani kuzijua Makala za Imani kumekusaidia wewe?

Siku moja shuleni, rafiki yangu Sophia aliniuliza ninaamini katika nini na kama nilikuwa wa dini yoyote. Ninaikumbuka ile Makala ya Imani ya kwanza, ambayo inasema, “Tunaamini katika Mungu, Baba wa Milele, na katika Mwanae,Yesu Kristo, na katika Roho Mtakatifu.” Hivyo nilishiriki hiyo pamoja naye.

Pia nilimwambia kwamba mimi ni Mkristo na muumini wa Kanisa la Yesu Kristo la Watakatifu wa Siku za Mwisho. Alinisikiliza na kunielewa kile nilichoshiriki pamoja naye.

Je, uzoefu huu ulikufanya uhisi namna gani?

Nilihisi vizuri sana kwa sababu nilijua kuwa nimekuwa jasiri kushiriki imani yangu pamoja na rafiki yangu. Kwa sababu ya kufanya kwangu kazi kwa bidii kujifunza Makala za Imani, niliweza kushiriki injili na kujua nini cha kusema.

Picha
Watoto wakiwa wamesimama pamoja
Picha
PDF ya hadithi

Vielelezo na Toby Newsome

Chapisha