Rafiki
Kumfuata Yesu huko Nikaragua
Julai 2024


“Kumfuta Yesu huko Nikaragua” Rafiki, Julai 2024, 6–7.

Kumfuata Yesu huko Nikaragua

Kutana na Felix!

Jinsi Felix Anavyomfuata Yesu

Picha
Picha ya Felix iliyopangwa katika vipande vya fumbo.

Felix anamfuata Yesu kwa kuwa mtiifu. Yeye anasali, anajaribu kushika amri na anaenda kanisani. “Ninajifunza mengi katika darasa la Watoto,” yeye anasema. “Kwenye darasa la Watoto, kuna watoto wengi sana na tunajifunza kuhusu Yesu Kristo.”

Felix anapenda kucheza pamoja na binamu zake. Lakini wakati mwingine yeye na binamu zake wanashindwa kuelewana. “Baba wa Mbinguni ananisaidia kuwa na subira,” yeye anasema.

Felix pia anawasaidia wenzake. Shuleni, Felix aliona kwamba wanafunzi wenzake wa darasa moja hawakuwa na vitafunwa. Felix aliwagawia wenzake vitafunwa vyake. Pia anamtunza dada yake mdogo. Anahakikisha yuko salama kwa kula vyakula vidogo vidogo tu.

Picha
Felix akiwa amevaa kofia na Felix akiwa anapiga kinanda.

Kuhusu Felix

Picha
Felix akitabasamu na kiputo cha usemi kisemacho ‘Hola’

Umri Miaka: 7

Kutoka: Managua, Nikaragua

Lugha: Kihispania

Lengo: 1) Kuwa mwanaanga na kwenda mwezini na pengine sayari ya Mars. 2) Kufuga kuku siku moja.

Mambo apendayo: Kujifunza kuhusu anga, kupiga kinanda na kupika.

Familia: Felix, Mama, Baba na dada mdogo

Mapendeleo yake

Hadithi ya Kitabu cha Mormoni: Wakati ambapo Yesu alipotembelea mabara ya Amerika na kuponya watu wote (3 Nefi 17)

Sikukuu: Krismasi

Tunda: Stroberi na tikiti maji

Rangi: Bluu

Wimbo wa Watoto: “I Will Walk with Jesus” (Rafiki, Feb. 2020, 27).

Picha
PDF ya hadithi

Chapisha