Rafiki
Uwekaji Wakfu Mahekalu ni Nini?
Julai 2024


“Uwekaji Wakfu Mahekalu ni Nini?” Rafiki, Julai 2024, 22.

Kadi za Mahekalu

Uwekaji Wakfu Mahekalu ni Nini?

Picha
PDF ya hadithi

Vielelezo na Rachel Erickson

Pale hekalu jipya linapomalizika, nabii au mtume anasema sala muhimu ili kuliweka wakfu, au kulibariki, hekalu hilo. Sala hii inaliweka hekalu maalumu kuwa mahali patakatifu ambapo sisi tunaweza kufanya kazi ya Mungu. Manabii wameahidi kwamba mamia ya mahekalu yatawekwa wakfu kwa Bwana.

Hekalu la Managua Nicaragua

  • Hili litakuwa hekalu la kwanza huko Nikaragua.

  • Mnamo 2012 Mzee Russell M. Nelson alitembelea Nicaragua na aliwasihi watu kujiandaa kwa ajili ya hekalu. Yeye alisema, “Ninakuahidini kwamba mtakapokuwa tayari, Bwana atafanya sehemu yake ili mpate hekalu” (ona Liahona, Juni 2012, 77).

Hekalu la Singapore

  • Hili litakuwa hekalu la kwanza katika Jamhuri ya Singapore.

  • Mwaka 2000, nabii aliwaalika waumini wa Kanisa huko Singapore kujiandaa kwa ajili ya hekalu.

  • Hadi litakapomalizika, waumini lazima wasafiri kwenda Ufilipino kuhudhuria hekalu.

Chapisha