Rafiki
Nini kipo Akilini Mwako?
Julai 2024


“Nini kipo Akilini Mwako?” Rafiki, Julai 2024, 38.

Nini kipo Akilini Mwako?

Ninahuzunika na kukasirika mambo yanapokuwa hayaendi jinsi ninavyotaka. Je, naweza kufanya nini?

—Quitting huko Quebec

Picha
Watoto wakionyesha hisia tofauti

Mpendwa Quitting,

Sisi sote tunahisi huzuni au hasira mambo yanapokuwa hayatokei kama tunavyotaka. Kumbuka kwamba Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wanakupenda na wanataka yaliyo bora kwako. Wanaweza kukusaidia ukiwa na hisia ngumu. Wakati mwingine tunakua zaidi wakati mambo yanapokuwa magumu.

Kama unaendelea kuhisi kukata tamaa, zungumza na mtu mzima unayemwamini. Kisha jaribu mojawapo ya mawazo haya. Andika mawazo yako mwenyewe pia.

“Mambo yatakuwa SAWA!

Gazeti la Rafiki

Kile ninachoweza Kufanya

  • Vuta pumzi ndefu na sali kwa ajili ya msaada.

  • Cheza nje au fanya kitu kingine ili kutuliza akili.

  • Andika au chora kuhusu hisia zangu.

  • _________________________________________________

  • _________________________________________________

Nini Ninachoweza Kusema

  • Baba wa Mbinguni na Yesu Kristo wananipenda na watanisaidia.

  • “Mimi ninajifunza, na ninaweza kujaribu tena.”

  • “Ninafanya ninaloweza, nami nitakuwa SAWA.”

  • _________________________________________________

  • _________________________________________________

Chapisha