“Ukumbi wa Maandiko,” Rafiki, Julai 2024, 14–15.
Ukumbi wa Maandiko
“Ingekuwaje kama tungetoka nje ya boksi la Jumapili?” Jonny alisema.
Hadithi hii ilitokea huko Marekani.
“Mimi nimechoka.” Jonny alilala sakafuni sebuleni.
Dada yake Jenna alikodoa macho nje ya dirisha. “Hakuna la kufanya,” alisema.
Jonny akitazama darini. Kwa nini inaonekana kama Jumapili sio za burudani?
Kisha aliwaza kuhusu kitu fulani. “Ingekuwaje kama tungetoka nje ya boksi la Jumapili?” Jonny alisema. Boksi la Jumapili lilikuwa ni boksi maalumu lililojazwa michezo ya kucheza siku ya Jumapili.
Uso wa Jenna uling’ara kwa tabasamu. “Hiyo ni burudani.”
Jonny na Jenna walikwenda haraka chumbani kwa mama. Wakaliburuza lile boksi kubwa hadi sebuleni.
“Tunapaswa kufanya nini kwanza?” Jonny alisema. Alifungua lile boksi na kutoa baadhi ya vitabu vya picha na kadi za michezo.
“Wacha tucheze mchezo wa kulinganisha maandiko,” Jenna alisema.
Mchezo ulikuwa na kadi zenye picha za manabii wa Kitabu cha Mormoni. Jenna alilaza zile kadi sakafuni uso ukiangalia chini sakafuni. Walifanya zamu ya kuokota kadi na kujaribu kutafuta inayofanana nayo.
Jonny aliokota kadi mbili tofauti na Kapteni Moroni akiwa juu yake. “Nimepata za kufanana!” alishangilia.
“Na mimi pia.” Jenna alishikilia kadi mbili zikimwonyesha Saria.
Jonny na Jenna walicheza michezo kadhaa zaidi. Ilikuwa burudani kufikiria kuhusu hadithi zao pendwa kutoka katika Kitabu cha Mormoni.
Baada ya muda Jenna alisema, “Na tufanye kitu kingine sasa.”
“SAWA. Wacha tuigize moja ya hadithi za maandiko tuyapendayo. Tutakuwa na ukumbi wa maandiko!” Jonny akaanza kuokota zile kadi.
“Ndiyo!” Jenna alisaidia kukusanya ile michezo na kuiweka mbali.
Jonny alichimba ndani ya lile boksi hadi akapata baadhi ya mavazi. Jonny alitoa vazi la kuchekesha rangi ya kahawia na kulivaa. “Mimi ni Samweli Mlamani!” Akarukia juu ya kiti na kuigiza kama Samweli , akifundisha juu ya ukuta wa jiji.
Jenna alifungua katika kitabu cha picha za Kitabu cha Mormoni. Alipekua kurasa mpaka akafika kwa Samweli Mlamani. Akasoma kwa sauti wakati Jonny akiigiza hadithi ile.
Watoto wale walifanyia mazoezi hadithi ile mara kadhaa. Jonny alipata hisia nzuri na furaha moyoni. Ilikuwa vyema kuwakumbuka manabii ambao walifundisha kuhusu Yesu Kristo.
Walipokuwa tayari, Jonny alikimbia na kumwita Mama, Baba na dada yao mdogo, Makenna. “Njooni muone mchezo wetu!”
Jenna alisimama katikati ya chumba mikono yake akiwa ameinyoosha. “Karibuni kwenye ukumbi wetu wa maandiko. Leo tutawasilisha hadithi ya . . . Samweli Mlamani”
Kisha Jenna akaanza hadithi. “Hapo zamani, nabii aliyeitwa Samweli alikuja kuwafundisha Wanefi . . .”
Ilipofika sehemu ya Jonny, alisimama akiwa mrefu juu ya kiti. Yeye alisema kwa sauti kubwa. “Mimi ni Samweli, na Baba wa Mbinguni anawataka ninyi mchague yaliyo mema. Muache kufanya mambo mabaya. Kwa sababu katika miaka mitano ijayo Yesu Kristo atazaliwa.”
“Nguvu za Mungu zilikuwa pamoja na Samweli,” Jenna alisema. Alimalizia kwa kusimulia hadithi yote. Ilipomalizika Mama, Baba na Makenna walipiga makofi.
Hiyo ilikuwa nzuri sana!” Mama alisema.
Jonny na Jenna waliinamisha vichwa. Walikuwa na tabasamu kubwa.
“Acha tufanye mchezo mwingine,” Jonny alisema.
“Tutapenda kuona mchezo mwingine,” Mama alisema. Makenna alipiga makofi na kutabasamu.
Jenna na Jonny walikimbilia kwenye boksi na kutoa mavazi mengine zaidi.
“Jumapili ni burudani! Napenda kujifunza kuhusu maandiko,” Jenna alisema.
“Na Yesu.” Jonny alitabasamu alipopata vazi jingine. Jumapili hakika ilikuwa siku maalumu!