Liahona
Dhahabu Safi
Julai 2024


Ujumbe wa Urais wa Eneo

Dhahabu Safi

Mara kadhaa katika maisha yangu, nimesikia mtu akitajwa kama dhahabu safi, ikimaanisha mtu ni wa thamani kubwa kwa sababu ya wema wao, upole na ukarimu wao. Inapendeza kuweza kufahamiana na mtu anayestahili sifa kama hiyo na nimekutana na watu wengi wa namna hiyo katika Eneo la Kati la Afrika. Hawa ni watu ambao wanajitahidi kila siku kuwa wanafunzi wa Kristo.

Nilipoacha shule katika shule ya upili mnamo 1971, [inaonekana kama kitambo sana] nilifanya kazi kama mkemia kwenye kampuni ya madini na nilifanya utafiti wa mawe kwa ajili ya kujua kiwango chake cha madini. Ilikuwa kazi yenye joto na vumbi lakini ya kuvutia ikiwa na uzoefu mwingi anuai. Kipengele kizuri zaidi cha kazi kilikuwa kwamba iliniruhusu nitunze pesa kwa ajili ya kuchangia kwenye gharama za misheni yangu. Mkemia mkuu nyakati zingine angewasha tanuru na kulipasha joto kwa zaidi ya nyuzi joto 1000 na kuweka ndani yake chombo cha udongo chenye mchanganyiko wa kimiminika na dhahabu yenye mawe. Matokeo yalikuwa kwamba aliweza kutengenisha uchafu mwingi ambao haukutakiwa na alibakiwa na dhahabu. Kadiri nilivyotafakari juu ya hili nimegundua pia kwamba kuna mchakato wa utakasaji kwa kila mmoja wetu.

Utakasaji wetu binafsi hauji kupitia kuwekwa ndani ya chombo na kuwekwa kwenye tanuru, bali kupitia uzoefu wetu wa duniani. Baadhi ya uzoefu huu unatusaidia, ikiwa tu radhi, kutupilia mbali kiburi na kwa unyenyekevu kumkubali Kristo kama Mkombozi wetu na kuishi kwa amri Zake. Utakasaji wetu mara nyingi huja kwa hatua na katika nyakati tofauti lakini hatuwezi kushindwa kamwe katika hali hizo. Mara nyingi ‘joto’ la uzoefu wa kutakasa ni zaidi ya vile ambavyo tungetaka, kama ilivyokuwa kwenye kazi, lakini tunapotoka nje ya ‘tanuru la kutakasa’ na tuko radhi kukubali masomo tuliyojifunza, tunakuwa bora zaidi kwa ajili ya uzoefu, kama alivyokuwa Ayubu. Isaya anasema “nimekutakasa, nimekuchagua kutoka kalibu ya masumbuko” (1 Nefi 20:10). Katika toleo la Kijerumani la mstari huo huo neno chaguliwa limetafsiriwa kama ‘tengenezwa’ ambayo hutupatia umaizi wa kuvutia kwenye malengo ya uzoefu wetu wa duniani ambao nyakati zingine ni mgumu.

Itakuwa upumbavu kuamini kwamba ni uzoefu mgumu tu ndio unatutakasa. Kadiri nilivyoshuhudia juu ya kweli za injili iliyorejeshwa nimehisi Roho Mtakatifu akinishuhudia juu ya ukweli wa kile nilichozungumza. Kadiri ambavyo nimesoma kutoka kwenye Kitabu cha Mormoni nimesikia ikithibitishwa kwangu hitaji la kufuata kile nilichokisoma na kadiri nilipowasikiliza viongozi wangu wa ukuhani nimehisi utumishi wao mtakatifu. Huu umekuwa uzoefu wa kutakasa wa upole na ukarimu; uzoefu ambao umeniacha nikihisi kuwa safi zaidi.

Thamani ya ziada inaongezwa kwenye dhahabu kadiri inaposanifiwa na wachongaji wenye ujuzi ili iwe vipande vya kidani cha urembo wa kuvutia. Bwana amewaweka ‘wachongaji’ kati yetu na ikiwa tu tutakuwa wanyenyekevu vya kutosha tutasanifiwa na kung’arishwa kikamilifu ili kutuwezesha turejee kwa Baba yetu wa Mbinguni. ‘Wachongaji’ wanaweza kuwa kiongozi wa Ukuhani au Muungano wa Usaidizi, pengine yeye atakuwa rafiki mwenye hekima, mwalimu, mzazi au Roho Mtakatifu. Bila kujali mchongaji ni nani, kuwa mwenye shukrani kwamba Bwana anakupenda sana kiasi kwamba anamweka mtu kama huyo kwenye njia yako. Ikumbuke ahadi Yake, ‘Jinyenyekeze; na Bwana Mungu wako atakuongoza kwa mkono, na kukupa jibu la sala zako’ (M&M 112:10).

Kadiri dhahabu inavyokaribia usafi mkamilifu inaongezeka katika uwezo wa kusanifiwa. Gramu 28 ya dhahabu inaweza kupigwa na kutengeneza skwea mita 17 katika kipande chembamba kinachoitwa karatasi ya dhahabu. Analojia ni kwamba kadiri tunavyoongezeka katika usafi na kuwa zaidi wa kuweza kusanifiwa kunakuwa na ongezeko katika jinsi Bwana anavyoweza kututumia ili kuimarisha ufalme Wake. Kanisa linakua kwa haraka katika Eneo la Kati la Afrika na hivyo tunahitaji waumini zaidi ambao ni wasafi kama dhahabu safi, wanafunzi wa kweli wa Kristo ambao wamevumilia kwa furaha moto wa mtakasaji na hivyo ‘wametengenezwa’ kukabiliana na changamoto na fursa zilizopo mbele yao.

Fahamu unapendwa na kukubalika kwa kile ambacho tayari unafanya ili kuujenga Ufalme wa Mungu duniani na kwa yale ambayo utayafanya mbeleni.

Chapisha