Liahona
Akidi za Ukuhani wa Haruni
Julai 2024


Dondoo za Kitabu cha Maelezo

Akidi za Ukuhani wa Haruni

Lengo na Muundo

Ukuhani wa Haruni huwasaidia watoto wa Mungu wajiandae kurejea kwenye uwepo Wake. Hushikilia “funguo za huduma za malaika, na za injili ya toba, na za ubatizo” (Mafundisho na Maagano 13; ona pia 3.3.2 katika kitabu hiki cha maelezo).

Lengo

Akidi za Ukuhani wa Haruni huwasaidia vijana wadogo wafanye na kutunza maagano matakatifu na wakuze uongofu wao kwa Yesu Kristo na injili Yake.

Akidi ni kundi lililopangiliwa la watu wenye ukuhani. Lengo la akidi ni kuwasaidia wenye ukuhani wafanye kazi kwa pamoja ili kushiriki katika kazi ya Mungu ya wokovu na kuinuliwa. Katika akidi zao, wenye Ukuhani wa Haruni huwatumikia wengine, hutimiza majukumu ya ukuhani, hujenga umoja na kuishi mafundisho.

Dhima ya Akidi ya Ukuhani wa Haruni

Dhima ya akidi ya Ukuhani wa Haruni huweza kumsaidia kila kijana mdogo aelewe utambulisho wake wa kiungu na lengo lake kama mtu mwenye ukuhani. Wavulana na viongozi wao hurejelea dhima mwanzoni mwa mikutano ya akidi na mikusanyiko mingine ya akidi. Dhima inasomeka hivi:

“Mimi ni mwana mpendwa wa Mungu na Yeye anayo kazi ya kufanya kwa ajili yangu.

“Kwa moyo, uwezo, akili na nguvu, nitampenda Mungu, nitashika maagano yangu, na kutumia ukuhani Wake ili kuwatumikia wengine, nikianzia nyumbani mwangu mwenyewe.

“Pale ninapojitahidi kutumikia, kutumia imani, kutubu na kujiboresha kila siku, nitastahili kupokea baraka za hekaluni na furaha ya kudumu ya injili.

“Nitajitayarisha kuwa mmsionari mwenye juhudi, mume mwaminifu na baba mwenye upendo kwa kuwa mfuasi wa kweli wa Yesu Kristo.

“Nitasaidia kuuandaa ulimwengu kwa ajili ya kurudi kwa Mwokozi kwa kuwaalika wote kuja kwa Kristo na kupokea baraka za Upatanisho Wake.”

Akidi

Askofu huwapangilia wenye Ukuhani wa Haruni kwenye akidi kama inavyoelezwa hapa chini. (Ona pia Mafundisho na Maagano 107:85–88.)

Akidi ya Mashemasi

Wavulana wanajiunga na akidi ya mashemasi kuanzia Januari ya mwaka wanapofikisha miaka 12. Katika umri huu pia wanafaa kuwa mashemasi kama wamejiandaa na wanastahili.

Mshiriki wa akidi ambaye ametawazwa kama shemasi anatumikia kama rais wa akidi. Pale inapofaa, mshauri mmoja au wawili na katibu wanaweza kutumikia pamoja naye. Washauri na katibu pia lazima wawe mashemasi.

Majukumu ya shemasi yameelezewa katika Mafundisho na Maagano 20:57–5984:111. Majukumu mengine yanajumuisha kupitisha sakramenti na kumsaidia askofu katika “kusimamia mambo ya kimwili” (Mafundisho na Maagano 107:68).

Akidi ya Walimu

Wavulana wanajiunga na akidi ya walimu kuanzia Januari ya mwaka wanapofikisha miaka 14. Katika umri huu pia wanafaa kutunukiwa kuwa waalimu kama wamejiandaa na wanastahili.

Mshiriki wa akidi ambaye ametawazwa kuwa mwalimu anatumikia kama rais wa akidi. Pale inapofaa, mshauri mmoja au wawili na katibu wanaweza kutumikia pamoja naye. Washauri na katibu lazima pia wawe walimu.

Walimu wana majukumu sawa na mashemasi. Pia huandaa sakramenti na kutumikia kama akina kaka wahudumu. Majukumu ya ziada yameelezwa katika Mafundisho na Maagano 20:53–5984:111.

Akidi ya Makuhani

Wavulana wanajiunga na akidi ya makuhani mnamo Januari ya mwaka wanapofikisha miaka 16. Katika umri huu pia wanafaa kutunukiwa kuwa makuhani kama wamejiandaa na wanastahili.

Askofu ndiye rais wa akidi ya makuhani (ona Mafundisho na Maagano 107:87–88). Askofu anaita mshiriki mmoja au wawili kutumikia kama wasaidizi. Katibu pia anaweza kuitwa. Wasaidizi na katibu wanapaswa wawe wametunukiwa kama makuhani.

Makuhani wana majukumu sawa kama ya mashemasi na walimu. Majukumu ya ziada yameelezwa katika Mafundisho na Maagano 20:46–52, 73–79.

Chapisha